Skip to content

“Nilifikia watu 1000 ndani ya mwaka mmoja”

Tshepang Basupi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kusini mwa Afrika wa Africa Inland Mission (AIM)
Nilipokuwa na miaka 14 nikiwa shule ya sekondari ya chini, nilihudhuria kambi ya Scripture Union na nikasikia injili kutoka Warumi 3. Ujumbe ule rahisi uliugusa moyo wangu, na nikampokea Kristo.
Nilikuwa na shauku ya kuwafikia wengine, hivyo niliweka malengo ya idadi ya watu nitakaowafikia ndani ya mwaka mmoja. Kwanza nilipanga kuwahubiria watu 300, na ikatokea. Kisha nikaweka lengo la kuwafikia watu 1000, na nikafanikiwa. Nilikuwa nikienda chumba kwa chumba nikihubiri kwa wanafunzi wenzangu.
Lakini kulikuwa na tatizo — nilihubiri, watu waliokoka, lakini baada ya miezi michache walikuwa wakiacha imani. Kulikuwa na kitu hakikuwa sawa. Hivyo niliamua kupata mafunzo ya jinsi ya kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Kristo.
Nilipata kijitabu na kukisoma, lakini hakikutosha. Rafiki yangu alinipa wazo la kwenda kwenye mafunzo ya umishenari. Nilienda kwenye mafunzo ya wiki sita yaliyoandaliwa na Ray Mensah, Mkurugenzi wa Afrika wa One Way Ministries. Nilisikia kuhusu makundi ya watu ambao hawajafikiwa, na Bwana alikuwa akitenda kazi moyoni mwangu.
Baadaye nilipata mafunzo ya umishenari kupitia CAPRO na nikahudumu kama mmishenari nchini Nigeria, Afrika Kusini, na Kenya. Kwa sasa ninahudumu Afrika Kusini.
Soma simulizi kamili kwa kiingereza hapa: https://afrigo.org/…/missionary-profile-tshepang-basupi/