“Nguvu ya sanaa” – Nyakati za wamisionari
Nilipokuwa mmishenari nchini Thailand, nilikuwa nikifundisha darasa la watu wa Thailand, ambao ni Wabudha, na kuimba nyimbo za Kikristo. Walipenda sana na walikubali nilipopendekeza niwafundishe kuimba kwa ishara za mikono. Na punde tu, wote wakaanza kuimba kwa ishara za mikono ya wimbo wa “Kuna Nguvu ndani Jina la Yesu.” Walikuwa watu 30, ambao hawajawahi kusikia jina la Yesu hata mara moja, walikuwa wakimsifu Mungu na huo ulikuwa ni wakati gani!
Nilipokuwa nikiwatazama, nilisema “Bwana, hatutakuja kujua nyakati kama hizi humaanisha nini kwa watu hawa ambao bado hawajafikiwa na injili.” Kulikuwa na nguvu kubwa mno, na baadhi yao walikuja na kutaka kujua zaidi kuhusu Yesu. Hii ilionyesha ushawishi mkubwa kwa njia ya sanaa/ubunifu.
-Mmishenari kutoka Afrika Kusini mpaka nchini Thailand