“Nafsi yangu inasukumwa kuwahubiri” – nyakati za wamishenari
Muhtasari: Daniel alikua kwenye maisha magumu sana hadi kumpelekea hali ya kutaka kujiua, lakini siku hiyo kabla hajameza vidonge, gafla sauti ikasikika redioni na mtangazaji akamhimiza ampokee Bwana. Aliokoka, na akaendelea kuhudhuria kanisani. Ingawa mambo hayakuwa rahisi, alivumilia na Bwana akaanza kumtumia Danieli kujenga ufalme wake.
Sehemu ya tatu kati ya tatu:
Hivi majuzi, nimekuwa na msukumo wa kuwafikia watu wa Asia. Imani yao ndiyo iliyonisukuma sana kuwahubiria injili kwa sababu ninajua wanajihusisha na miungu ya uongo. Kwasababu hii, nafsi yangu inasukumwa kuwahubiria habari za Yesu ingawa najua kwamba ni kazi ngumu. Nimesikia mara nyingi kwamba baadhi ya Wahindi wanapoingia Ukristo, wanateswa na kutengwa na hata kuuawa.
Lakini, ninatiwa moyo na Maandiko yanayosema kwamba ni kwa ajili yao pia kwamba Yesu Kristo alizaliwa. Wahindi wako katika moyo wa Mungu na anataka waokolewe. Mtume Paulo alisema, “Ole wangu nisipoihubiri Injili. Tunapokuwa nao, tunaona kabisa kwamba wanahitaji injili kweli.
Hivi sasa, nina marafiki wachache wa Kihindi; baadhi yao wanakiri kwamba kweli hawajaokoka, lakini baadhi yao pia wameokoka kabisa na wengine wanataka kubatizwa kwa siri kwa sababu zao binafsi, lakini bado sina mamlaka ya kufanya hivyo.
Wanaenda kanisani kwa siri au kuhudhuria nyakati za maombi. Rafiki yangu mmoja huwa anajifanya Kwenda mazoezini lakini badala yake, huungana nasi kwenye maombi. Anasema inamlazimu awe msiri kwa sababu anaogopa mtu yeyote kugundua kwamba amebadili dini kuwa Mkristo. Wanahitaji maombi yetu na kutiwa moyo. Ninaamini kwamba kwa kila Mhindi mmoja aliyeokoka anaweza kuongoza angalau Wahindi kumi pale Mungu anapokuwa anafanya kazi nao.
Wanahitaji mapenzi, wanahitaji nguvu, lakini haswa wanamhitaji Mungu kusema nao, kwa sababu kikwazo kimoja tunachokabiliana nacho katika kuhubiri Wahindi wa Madagaska ni swali hili, ‘Ikiwa Mungu wako anaokoa, inakuwaje kwa nini wewe ni maskini?
Kila mtu ana nguvu kwenye wito wake kwa sababu Mungu ana njia isiyoeleweka ya kumtumia kila mtu.
Neema na rehema kwako,
Ushuhuda kutoka kwa Tsimavandy Daniel, Mmisionari wa Malagasi
Picha ya mwakilishi kutoka AIM Stories