Skip to content

“Nadhani nitakuja kuwa Mkristo” – nyakati za wamishenari

Mimi ni miongoni mwa watu wachache sana waliolipwa kusikia injili. Nilikuwa mwalimu wa lugha, nikifundisha watu wazima hasa wageni kama wamishenari kuongea Kiswahili. Sikuwa Mkristo, na nilidhani hii ilikuwa njia rahisi ya kupata pesa.
Niliwafundisha wamishenari kila siku kwa muda wa masaa mawili. Kadri nilivyoendelea kutafsiri na kuwafundisha, nilianza kuvutiwa sana na mambo niliyokuwa nayasikia. Siku moja nilienda nyumbani nikamwambia mke wangu, “Nadhani nitakuja kuwa Mkristo!”
Baada ya muda, nilimkabidhi maisha yangu Kristo! Hivi karibuni, niliingia katika Chuo cha Theolojia cha Scott (sasa kinaitwa Chuo Kikuu cha Kikristo cha Scott) nchini Kenya.
Nilijawa na msukumo moyoni mwangu kuwa mmishenari pia. Nilitamani kujifunza na kufundisha wengine kama vile mimi nilivyofikiwa na kufundishwa. Nilitamani kushiriki katika kazi ya kutafsiri na kuwafikia Waislamu. Zana/machapisho nilizokuwa nikisaidia kutafsiri vilinionyesha hitaji kubwa la mafunzo kwa wamishenari walioitwa kuwafikia Waislamu.
Baada ya chuo, niliomba kufanya mafunzo kwa vitendo na Life Challenge Africa (LCA) ili kuchunguza kama Bwana angeniongoza katika huduma hiyo. Ndani ya wiki mbili tu za mafunzo ya miezi mitatu, nilijua kabisa kuwa hii ndio huduma niliyotaka kufanya.
Nimekuwa nikifanya kazi na Life Challenge Africa (LCA) kwa miaka 20 sasa – nikifundisha, kutoa mafunzo, na kutafsiri zana/machapisho ya injili. Mke wangu alifariki miaka sita iliyopita kutokana na matatizo ya kisukari, lakini naendelea na huduma hii nikiwa mgane. Mtoto wangu wa mwisho ana miaka kumi na sita. Makanisa sasa yanapokea mafunzo kwa moyo mkunjufu zaidi, jambo ambalo ninamshukuru Mungu sana.
LCA ni huduma inayotafuta kushirikiana na Wakristo wote wanaotamani kutii Agizo Kuu la Kristo na walio tayari kuwafikia Waislamu kwa ajili ya Kristo katika maeneo maalum. Kwa sasa, mimi ni Naibu Kiongozi wa Timu, Mratibu wa Mafunzo, pamoja na Afisa wa Mahusiano ya Umma katika LCA.
Soma hadithi yote kwa Kiingereza kupitia https://afrigo.org/story…/missionary-profile-jared-oginga/
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us