“Kwa nini unaishi duniani?” – nyakati za wamishenari

Tariku Gebre – Sehemu ya 1 kati ya 2
Nikiwa na umri wa miaka 8, nilialikwa na rafiki yangu kuhudhuria shule yao ya Jumapili. Familia ya rafiki yangu ilikuwa ya kiinjili na hivyo walitazamwa na serikali pamoja na kanisa la Orthodox kama waovu na wafuasi wa “dini ya kuagizwa kutoka nje.”
Licha ya maonyo ya mara kwa mara kutoka kwa familia yangu ya Kiorthodoksi ya jadi, niliendelea kuhudhuria shule ya Jumapili kwa zaidi ya miaka miwili bila wao kujua. Uzoefu huu wa utotoni uliniachia msimamo wa dhati juu ya uwepo wa Mungu, nikimtambua kama Muumba.
Tukio langu la kukutana na ukweli, ulionileta kwenye uhusiano wa kibinafsi na Mungu, lilitokea nilipokuwa mwanafunzi wa kidato cha mwisho katika shule ya sekondari. Siku moja alasiri, nilipokuwa nikirejea nyumbani kutoka shuleni, nilisikia sauti ya upole na utulivu.
“Tariku, kwa nini unaishi duniani?” nisingeweza kusema kama mtu mwingine angeisikia sauti hiyo kama angekuwa nami. Lakini kwangu, ilikuwa ya wazi na yenye nguvu, kana kwamba imetamkwa na mamlaka fulani iliyokuwa na haki ya kupata jibu papo hapo.
Nilianza safari ya kutafuta jibu la swali hili nililoulizwa. Baada ya miezi sita, kupitia ushuhuda wa uaminifu wa msichana mmoja mdogo wa Kiinjili, nilipata jibu langu: Nimeumbwa ili niishi kwa ajili ya Mungu, na njia ya kumfikia Mungu ni kupitia Kristo Yesu.
Hivi karibuni nilipata kuanza kutumika katika nafasi ya Mkurugenzi wa Afrika kupitia Horn of Africa (USA). Shauku na tamanio la moyo wangu ni kuongeza uwezo wa Kanisa la Afrika katika kulituma kundi lake kutimiza jukumu la kuwafikia wasiofikiwa. Tunatamani kuona Afrika ikibadilika, ikiwa na vituo vya kutuma wamishenari vilivyotapakaa kote barani.
Tariku Gebre, Mkurugenzi wa Afrika, Huduma ya Horn of Africa.
Soma hadithi yote kwa Kiingereza https://afrigo.org/…/missionary-profile-tariku-gebre/…