Skip to content

Kuhamasisha Umishenari Afrika ya Kaskazini

Mike Adegbile
Niliokoka nikiwa na miaka 14, na muda mfupi baadaye kueneza Injili likawa jambo la kawaida kwangu. Uhusiano wangu na Scripture Union ulinisukuma kueneza Injili miongoni mwa wanafunzi. Nilikuwa na hamu ya kujua Mungu alikuwa anafanya nini duniani na jinsi ambavyo ningeweza kushiriki. Nilienda katika safari yangu ya kwanza ya umishenari wa kuvuka kwenda tamaduni nyingine huko Togo.
Baadaye nilijihusisha na kundi lililoitwa World-Wide Jesus Crusade (WWJC). Kiongozi wa timu hiyo alianza huduma ambayo ilipanua maono yangu na kunipa mtazamo mpana zaidi wa maono ya Mungu kwa ulimwengu, hasa kwa ulimwengu wa Kiislamu.
Nilipoingia katika uongozi wa Nigeria Evangelical Mission Association (NEMA), nilianza kusoma kuhusu ulimwengu wa Kiislamu, jambo lililochochea moyo wangu kwa ajili ya Bwana. Sehemu ya Kaskazini kwa kiasi kikubwa ina watu wa dini ya Kiislamu na hakukuwa na kazi nyingi za Injili zilizokuwa zikifanyika. Nilianza kujifunza kwa kina kuhusu nchi za Afrika, na nikahisi mzigo moyoni kuona kwamba Injili bado haijawafikia watu katika sehemu hiyo ya bara la Africa.
Sasa mimi ni kichocheo cha umishenari (mission catalyst), nikihamasisha nguvu ya Wainjilisti wa Afrika ili kuwafikia watu wa Afrika ya Kaskazini.
Soma hadithi kamili kwa kiingereza hapa:
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us