fbpx Skip to content

“Kufanya wanafunzi kuanzia chini kwenda juu”

Nimepunguza namba zangu nyingi za simu mpaka watu kumi na moja, kufuasa kwa ukaribu, kuandaa na kufundisha. Ufuasaji ni vurugu na kujitoa kutembea kwa ukaribu na watu hawa ni jaribu la uvumilivu wangu, kuamua, na hata Imani yangu katika mchakato wa ufuasaji kwa utimilifu wake. Katikati ya yote,jambo kubwa linalonipa moyo ni kusikia shuhuda zao kwa namna gani walivyomsikia BWANA kwa mara ya kwanza na kwa namna gani anavyofanya kazi maishani mwao.

Watu hawa wanasema walisikia kuhusu Yesu lakini walishindwa vuka mpaka kwa sababu kila aliyewapelekea Injili aliwaacha pasipo kuwafatilia. Hili lilikua gumu kwa sababu kulikua hakuna makanisa kwenye vijiji vyao au wanafunzi waliojulikana ambapo wangeweza kupata mafundisho yoyote au ushirika. Weng walirudi nyuma ingawa walionekana kupenda kile walichokisikia. Wanashukuru kwa kujihusisha nao kwa maandiko kwenye kujisomea Biblia Pamoja imekua msaada kwa wao kuielewa Injili.

Ninaendelea kukumbushwa kwa juu ya wito wa Mungu kwa waamini wote- kufanya wanafunzi na si tuu mtu aliyebadili dini, kuwafundisha na kutembea pamoja kwenye ukomavu. Paulo alisema ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo” Wakolosai 1:28

-Timothy Babweteera

Picha: AIM Stories

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us