Skip to content

“Kila mmoja wetu aliona aibu” – nyakati za wamishenari

Kupishana kwetu kiutamaduni ilikuwa ni kitu kilichonipa ugumu wakati wangu nikiwa katika kundi la watu wenye miiko mikali ya kitamaduni na udhibiti mkubwa wa maisha ya wanawake na wasichana. Wakati sisi wafanyakazi wa afya ambao ni Wakristo tulitaka kuzungumza na wasichana kuhusu usafi wa hedhi, tulimwomba mama mmoja ambaye ni mwenyeji kuwakusanya na kuandaa kikao. Kwa bahati mbaya wanaume wa jamii ya hapo walikuwa na mashaka juu ya kile tunachoweza kuwaeleza wasichana hao! Tulipaswa kupata ruhusa kutoka kwa kiongozi, ambaye angeweza kujua mipango yetu na kutoa ruhusa.
Badala yake, kila mtu aliona aibu na ilikuwa ni hali ambayo sasa sio rafiki kwani kikao kilisimamishwa ghafla na wanaume hao ili tuwaeleze tunazungumza nini. Baada ya hapo, tuliendelea kufanya kazi yetu kwa umakini zaidi na unyenyekevu. Lakini, kulikuwa na mambo muhimu mengi ambayo yalijitokeza wakati nikiwa huko. Tuliwashuhudia juu ya imani baadhi ya watu waliokubali, tuliweza kuishi pamoja na wanajamii mbalimbali, na ilifurahisha sana kuona wasichana wakitabasamu kwani walipata ushauri mzuri na msaada kuhusu usafi.
– Mfanyakazi wa afya kutoka Uganda aliyehudumu katika jamii ya Kiislamu – Afrika Mashariki
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us