“Kiboko kwenye ndoo”- nyakati za wamisionari
Tulikuwa katika kijiji kidogo nchini Msumbiji kwa miezi michache kuendesha mafunzo ya ufuasi. Asubuhi moja tuliamka na vijana wakaenda mtoni ambako walinunua nyama ya kiboko kwa kijana mmoja, kwa chakula cha mchana. Kulikuwa na jengo dogo la choo cha duara, na kabla hatujaondoka kwenda kuhubiri nilimwona mama mwenye nyumba akifanya usafi kwenye choo hicho. Alikuwa akitumbukiza kitambaa kwenye kwenye ndoo ya maji na kuipangusa sakafu, na kuchovya kitambaa tena na kukikunja. Sikufikiria sana wakati huo.
Tuliporudi baada ya uinjilisti tulikuwa tumechoka sana na tulikuwa na njaa ya chakula cha mchana cha nyama kiboko, je tuligundua nini? Tulikuta nyama ya kiboko imepikwa na kujazwa kwenye ndoo ileile ambayo ilikuwa imetumika kusafisha choo. Tulipatwa na mshtuko mkubwa. Lakini, hatukusema chochote ikatulazimu tu kula nyama ile. Hatukuweza kufanya chochote! Hatukuweza kupoteza nyama ambayo ilikuwa nadra kupata. Kwenye maeneo kama hayo, ambayo watu wanauhitaji sana, huwezi kutupa chakula. Ilitubidi tu tuombe na kumwamini Mungu atalinda afya zetu na vijidudu au magonjwa yoyote kutokana na tuliyokula nyama hii. Tulikula na tukapata chakula kizuri cha mchana na niko hapa leo kusimulia hadithi.
-Mmishenari kutoka Zambia nchini Msumbiji