Skip to content

“Kesi nyingi za Ebola na vifo” – nyakati za wamishenari

Nilihisi mzigo mzito wa kujitolea maisha yangu yote kwenye kazi ya umishenari baada ya kumaliza masomo yangu ya chuo kikuu.
Nilikubali kufanya kazi ya ualimu huko Bo, jiji la pili kwa ukubwa nchini Sierra Leone, ambako pia nilifanya sehemu kubwa ya kazi yangu ya umishenari kama mwalimu wa Kiingereza katika shule ya msingi. Nilipoamua kwenda katika safari hii ya kimishenari, hofu ya familia yangu ilikuwa hasa kwa sababu ilikuwa nchi ya kigeni ambapo hakukuwa na mtu yeyote wa kumtegemea iwapo kitu chochote kitatokea.
Ilikuwa ngumu kwa familia yangu kuniruhusu kwenda safari ya misheni hii, hasa mama na baba yangu, kwa sababu walihisi kuwa nilikuwa mdogo sana kufanya safari ya aina hii. Nilijua kuwa nilipaswa kuitikia wito huu, hivyo niliweka kila kitu katika maombi kwa Bwana, naye Bwana alijibu. Hatimaye nilipokea baraka za familia yangu kwa ajili ya safari hii ya kimishenari na nikaenda kufanya huduma. Hata hivyo, nililazimika kufupisha safari hii kwa sababu Sierra Leone ilikuwa imeripoti visa vingi vya Ebola na vifo kuanzia mwaka 2013 hadi mwanzoni mwa 2014.
Janga la Ebola lilileta hofu kubwa kwa familia yangu, na walizidi kushawishika kuwa nilipaswa kurudi Ghana. Kwa upande wa nje na familia, nilikumbana na upinzani kutoka kwa baadhi ya marafiki zangu. Marafiki wawili wa karibu sana walionesha kutoridhika kwao kwa kusema kuwa nimewaangusha kwa kuacha kufanya yangu ya kulitumikia Taifa na kusafiri kwenda katika taifa la Kiislamu kuhubiri, wakijua kuwa maisha yangu yangekuwa hatarini.
Mara nyingi huwa rahisi zaidi kusafiri au kutumikia tukiwa na wengine na kutegemea nguvu za watu wengine, lakini kuna nguvu kuu zaidi na matokeo mengi zaidi tunapomtegemea Bwana peke yake. Kwa kufanya hivyo, huvuna mavuno mengi zaidi kwa ajili ya Bwana. Hamasa yangu kuu ni kwa vijana, hasa wasichana: naamini kuwa Mungu ametupa uwezo mkubwa, na tunaweza kumtumikia Bwana zaidi tunapokuwa hatuna watoto wa kulea, mume wa kumheshimu na kumtii, wala nyumba ya kuisimamia.
Naamini kwamba Mungu huchagua yule anayemtaka kumtumia kwa wakati wowote ule, bila kujali kabila, jinsia, lugha, au tamaduni zake. Kile ambacho Bwana anahitaji kutoka kwetu ni moyo wa kujitolea usemao: “Bwana, niko tayari: nitume, nami nitaenda.”
Soma hadithi yote kwa Kiingereza kupitia hapa https://afrigo.org/stor…/missionary-profile-deborah-sekyi/
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us