“Hata wanawake waliruhusiwa kucheza!”-nyakati za wamishenari
Ambassadors Football International, kupitia ushirikiano na mojawapo ya Makanisa makubwa ya Wapentekoste (ADEPR) nchini Rwanda, yalianzisha programu za kandanda ya mtaa mwaka 2017 ili kufikisha injili ya Yesu kwa watoto. Sasa, zaidi ya watoto 6000 wanashiriki kila wiki. Ingawa huduma imekuwa na mafanikio makubwa, lakini ilianza kwa ugumu. Kanisa lilikuwa linalinda sana utamaduni wake na halikuamini katika michezo au kuruhusu wanawake kuvaa suruali au kaptura kucheza mpira wa miguu.
Kwa hiyo, Mabalozi walianza mafunzo kwa ngazi ya juu ya uongozi wa kanisa, wakiwakumbusha ushauri wa Paulo katika 1 Wakorintho 9:22b: “Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu.” Ili kuwafikia vijana ambao walikuwa hawaji kanisani, lazima watu wawe watu wa michezo ili waweze kuwavutia vijana ambao wapenda michezo. Walionyesha mfano wa huduma ya mwili kwa viongozi, na kwa ruhusa yao walianza kidogo kidogo, waliomba kanisa litume watu/vijana wao walio wazuri kwenye michezo ili kwa namna hiyo waifikie jamii. Hatimaye, hata wanawake waliruhusiwa kujiunga – na kuvaa suruali!
Mabalozi walisisitiza Kandanda (Mpira wa miguu), Imani na Kesho iliyo bora, na lengo la kila mkusanyiko ni Kujifunza Biblia pamoja na michezo na uchezaji. Watoto wadogo wanahimizwa kukariri Maandiko (Mistari). Sasa, ni moja ya programu kubwa Afrika!
Jean Paul Seneza, Mkurugenzi wa Ambassadors Football Africa