“Dada yangu aliniambia ninapoteza muda wangu” – nyakati za wamishenari

Familia yangu haikukubaliana na uamuzi wangu na waliendelea kujiuliza sana kwamba nimepoteza ufahamu. Shangazi yangu alisema, “Kazi ya umishenari ni ya watu ambao tayari wamejipanga na wameweka akiba ya pesa za kutosha kujikimu.” Dada yangu aliniambia kuwa ninapoteza muda wangu.
Kauli hizi zilinisumbua na mwishowe, ilinibidi kuzima simu yangu baada ya kuwa nimeenda kuanza kazi hata bila kupata msaada wote niliohitaji. Licha ya vikwazo hivyo vyangu binafsi, wamishenari wenzangu na mimi tuliweza kuanzisha ushirika wa pamoja ambapo tunakutana kila Jumatano na kushirikishana injili.
Hatimaye, familia yangu walikubali kwamba nilikuwa nimeamua kumtumikia Mungu na kuelekea mwishoni mwa mwaka wa kwanza wa misheni, nilipata msaada kutoka kwa baba yangu. Tangu wakati huo, wanaelewa vizuri kujitoa kwangu kwa ajili ya wito wa Mungu juu ya maisha yangu. Baada ya misheni hiyo ya kwanza, niliendelea tena kwa mwaka mwingine miongoni mwa kundi gumu la watu wa Kiislamu katika nchi ya kigeni ambapo inawezekana tu kuingia katika nchi kwa kigezo cha ujuzi wa kitaaluma na si kama mmishenari. Namshukuru Mungu kwa nafasi ya kumtumikia na ninaomba juu ya kile ambacho ataandaa kwa ajili yangu mbeleni!!
-Muuguzi mmishenari Mu-Uganda
Picha ya mwakilishi