fbpx Skip to content

“Aliwakodolea macho wamisionari” – nyakati za wamisionari

Ghadhabu ya adui shetani ilikuwa kali mno miongoni mwa watu wa Kiislamu haswa Kaskazini mwa nchi ya Nigeria. Ilikuwa ni kama vita. Timu yetu ya misheni ilipata mashambulizi na upinzani mwingi wa kuzimu. Walipambana na nyoka na nguvu za giza. Siku moja, nyoka mkubwa alitokea kwenye boma lao. Macho yake yaling’aa alipowatazama wamishenari. Walitoa wito kwa wanakijiji kusaidia kumuua. Lakini, wanakijiji walisema, “Msimuue!. Kwani hajawafanya lolote.” “Yule nyoka aliendelea kusimama pale hakuwa na haraka ya kwenda, alikuwa anatutazama tu. Mmoja wa wanakijiji akazungumza na nyoka ndipo akaondoka. Tuliwaambia kwamba nyoka huyo akija tena hataondoka, kwa sababu tulidhamiria kumuua. Siku chache baadaye, tukamuua nyoka yule na alikuwa kaingia ndani ya nyumba. Lakini, watu waliomuua nyoka huyo wakaanza kuumwa.

Kundi la watu hawa lilikuwa likijigamba kwa kundi la Wafulani kwamba baba yao ni mfuasi wa Mtume Muhammad, na kwamba wao ni wamiliki wa dini hiyo kwa sababu hawakuipata kwa njia ya vita kama Wafulani. Walijigamba kwamba hakuna hata mmoja wao ambaye angeacha imani hiyo na kuwa mkristo na hata walifika hatua ya kuwashawishi wamishenari wetu kuifuata imani ya Kiislamu. Wamishenari wetu waishio kati yao walitangaza siku za maombi, pamoja na mikesha ya maombi. Baada ya muda, Mungu alionekana kati ya watu hawa na kuanza kupata wafuasi wapya.

Yesu alikuwa akiwatokea watu kwenye ndoto. Wakaanza kusema walimwona mtu aliyevaa nguo nyeupe, na uso wa utukufu. Wamishenari wakatumia nafasi hiyo hiyo hilo kuwashirikisha Injili. Mwanamke mmoja aliyeokoa alitokwa na pepo la ukichaa ambalo alikuwa nalo tangu utoto. Kuna mtoto mwingine ambaye alikuwa hawezi kusimama wala kutembea. Baada ya maombi, mtoto huyo wa miaka 12 alifunguliwa na kuinuka. Watu waliokuwa wamelazwa au kupelekwa hospitalini bila kupata nafuu yoyote walipata nafuu na kupona baada ya maombi. Waumini wapya waliwaombea vichaa watatu na wote waliponywa. Mwanamke aliyekuwa na tatizo la kutokwa na damu kwa muda wa miaka mitatu aliombewa na wanawake waliokuwa wameenda kuhubiri injili na akapona. Kuna mtu mwingine alimleta mwanawe kichaa kwenye maombi. Na yeye pia aliponywa. Baadhi ya waumini wapya hawa wamekuwa walimu na wanamtumainia Mungu. Leo hii wana makanisa machache ya nyumbani, ambayo baadhi yao hukutana kwa siri nyakati za usiku.

Kutoka kwenye jarida la Occupy la CAPRO toleo la 45.2 “Kilio cha kondoo wengine” na Festus Ndukwe

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us