fbpx Skip to content

“Alirudi akiwa na panga” – nyakati za wamishenari

Juma mosi moja asubuhi, nilienda sokoni kama kawaida kununua mboga/vyakula, na nilivyokuwa nikifunga vitu kwenye pikipiki, niliona ugomvi. Vijana wawili walikuwa wakisumbua na kumshambulia kijana mwingine. Watu walijaribu kuingilia kati, nami nikajiunga ili kuona kama tunaweza kuwazuia hao wawili kumnyanyasa yule kijana mwingine.
Waliendelea kufanya hivyo kwa muda, wakirusha matusi na kumpiga yule mtu asiyejiweza. Kisha mmoja wao akaondoka, akarudi akiwa na panga. Nilijaribu kuingilia tena, lakini walikuwa nia ya kumdhuru kijana huyo.
Ndani ya sekunde chache, mwathiriwa aliondoka haraka na pikipiki yake na kutuacha sisi wengine nyuma. Kwa kuwa walikuwa wanahasira, washambuliaji walinigeukia. Mara ghafla nilipigwa na panga mkono wa kushoto huku nikijaribu kumzuia asipige kichwa changu. Nilijua lazima nikimbie. Tuliondoka, mimi mbio kuokoa maisha yangu na yeye moto chini, akipiga kelele kwa ajili ya damu yangu.
Nilipita katikati ya magari kutokana na msongamano wa magari. Nilijikwaa na kuanguka mara mbili, hio ikimwezeshakufika kwangu. Alinipiga mara mbili kwenye mapaja yangu. Kila kitu kilianguka kutoka mfukoni mwangu, na kwa kushangaza vijana walichukua sarafu ya shilingi 20 ya Kenya, na kuacha simu yangu ya mkononi iliyokuwa karibu nami.
Nikiwa chini, katikati ya mji wa Garissa, nikipumua na kukumbuka kilichonipata muda mchache, nikitazama chini mkono wangu unaovuja damu na suruali iliyochanika. Umati ulianza kuongezeka karibu yangu, wakiuliza ni nini kilikuwa kimetokea. Sikuweza kuongea. Akili yangu ilikuwa mbio napumzi yangu ikiwa nzito. Ghafla, taa iliwaka kichwani mwangu – hii ni fursa nzuri ya kuhubiri injili!
Nilipata utulivu haraka na kusimulia matukio kwa umati, ambao ulikuwa sasa na wasiwasi. Hii ilikuwa mara ya pili nilipata umati wa watu waliokuwa wakisikiliza kwa makini kabisa huko Garissa. Niliwashirikisha kuhusu mafundisho ya Yesu juu ya baraka za wapatanishi.
Tukio hili lilinikumbusha matukio kadhaa ambapo karibu wampige mawe Mwokozi na Bwana wetu lakini wasingeweza kufanya hivyo, kwa sababu tu haukuwa wakati wake (Yohana 8:20). Ilinipa ujasiri wa kujua kwamba hakuna madhara yoyote yatakayotupata isipokuwa jinsi Bwana anavyoweza kuruhusu kwa utukufu Wake.
Joseph Otieno, mmishenari nchini Kenya kutoka taifa la Wajaluo akihudumu katika Kanisa la In Christ Church International (ICCI) miongoni mwa watu wa Somalia, Kaskazini Mashariki mwa Kenya.
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us