fbpx Skip to content

“Alikufa pamoja na furaha kuu”- nyakati za wamisionari

Juma lililopita, kaka yetu mnaijeria, akiwa ametoka kwenye shule ya umishenari alisafiri pamoja na wenzake kuelekea mbali ambapo walikutana mishangao ya halisi ya kiutamaduni. Habari inaendelea:

Vyakula vyao havikuwa vile tulivyozoea. Nafaka zilijulikana, lakini maandalizi yalikuwa ya aina yake. Vivyo hivyo, maji yalikuwa ya rangi ya maziwa. Lakini tulifundishwa jinsi ya kuishi kwenye tofauti ya utamaduni, kwa hiyo tuliwakubali watu na vyakula vyao, tukamwamini Mungu kwa Maisha yetu, tukabariki chakula na maji, na kula chakula chetu kwa furaha na nyakati fulani kwa shida zaidi.

Tulimlenga kijana aliyeitwa Babangida wa karibu miaka 19 ambaye alikuwa ametoka kuoa msichana mrembo, ambaye alikuwa akitufatilia mara kwa mara. Alijifunga kanga yake kifuani, lakini alikuwa akiitupa kila alipotuona, akitufuata na kutafuta njia ya kujionyesha kwetu hata mumewe akiwepo. Alinilenga mimi, na mwishowe nilimkemea vikali mbele ya mumewe, ambaye hakuonekana kujali, lakini hiyo ilimaliza usumbufu.

Tuliwakusanya vijana wao kuungana nasi kuchimba kisima na baada ya majuma mawili tukapata maji. Hii ilileta furaha kubwa kwa watu. Tulihubiri katika kila eneo kwenye jumuiya hii, tukienea hadi kule kule. Wengi waliikataa injili tulipowahubiri kumkubali Kristo, lakini miezi 20 baadaye, niliamua kurudi ili kutumia siku yangu ya kuzaliwa pamoja nao na kutembelea tena kazi hiyo. Nilijawa na furaha sana nilipogundua wengi wao waliomkataa BWANA walikuwa waamini na walikua wamebatizwa.

Kesi moja ya kushangaza ilikuwa ya ajuza. Baada ya sisi kuhubiri injili, alisema alikuwa akipendana na mume wa ujana wake ambaye alikuwa amekufa na kwamba ikiwa atamkubali Yesu alihofia kwamba huenda asingemwona tena katika maisha yajayo. Hivyo aliomba tumsamehe. Lakini niliporudi, niliambiwa jinsi alivyoikubali injili na kufa kwa imani kwa furaha, akiwaambia wajukuu zake kwamba wakati wowote watakaponiona tena wanijulishe kwamba Yesu wangu amekuwa BWANA wake kabla hajafa na kwamba alikufa pamoja na furaha kuu.

Hii ilikuwa safari yangu ya kwanza ya umisheni baada ya mafunzo na ilikuwa maandalizi mazuri kwa kazi yangu ya thamani katika misheni.

-Kaka Ugochukwu G.U. ni mmisionari toka CAPRO akiwafikia waislamu wahamiaji wa kaskazini walioko mashariki ya Nigeria.

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us