fbpx Skip to content

Wachungaji Ni Ufunguo Wa Maono Ya Kanisa juu Ya Umisheni

Mungu amewachagua wachungaji ili kulielekeza na kuliongoza kanisa lake. Ni maono na kielelezo cha Mchungaji ambacho kitalielekeza kanisa na ushiriki wake katika umisheni. Kama unaongoza kanisa unaweza kulisaidia kusanyiko kufahamu na kupokea jukumu lake kwa ajili ya umisheni wa ndani na nje ya nchi. Kila mmoja anapaswa kujua kwamba sisi sote tuna sehemu ya kufanya katika mpango wa Mungu wa umisheni.

Unaweza kumtia moyo kila mkristo kanisani kwako ili ashiriki katika umisheni kwa kwenda au kutuma (kupitia kuomba na kutoa).

Fikiria juu ya kuhubiri ujumbe wa kimishenari kwa watu wa Mungu kila upatapo nafasi. Kanisa lako linaweza kuwa na kamati au mpango wa umisheni, lakini usiunde kamati ya kufanya yale ambayo kanisa lote linapaswa kufanya! Huu ndiyo mwanzo mkuu! Bila kujali lilipo kanisa lako kwa sasa, mara zote huwa kuna hatua za kuchukua pale inapokuja katika kufanya umisheni wa kuvuka utamaduni mmoja kwenda mwingine. Unaweza kusaidia wakristo wako kufika mahali ambapo watu wanaweza kusema, “Sisi ni kanisa linalojali na kufanya umisheni” na si kwamba “sisi tuwe ni kanisa lenye mipango ya umisheni tu” bali kutumika katika kazi za umisheni isiwe ni kitu cha kujadiliwa na watu sita tu katika ofisi ya kanisa.

Itakuwa ni jambo jema kiasi gani kama suala hili litakuwa katika kinywa cha kila mtu katika kusanyiko lote la kanisa! Badala ya umisheni wa kiulimwengu kujielekeza kwenye juma moja tu kila mwaka katika kampeni au kufanya kongamano kubwa, kwa nini msifuatilie kupata taarifa na changamoto za umisheni kipindi chote cha mwaka?

Safari za umisheni siyo tu kwa ajili ya makundi ya vijana. Bali ni Safari za kulitembelea kundi la watu ambao wanaishi na kufa bila Kristo katika nchi yako au katika nchi nyingine za jirani ili kufungua macho ya watu na kupanua maono yao. Wape washirika wa kanisa lako nafasi ya kushiriki katika safari za umisheni – ni safari za kubadilisha maisha!

Haya hapa ni baadhi ya mawazo na mapendekezo ya kukusaidia kuliwezesha kanisa lako:

 

 

  • Fanya kongamano la umisheni kwa kuwaalika wamishenari ili kutia moyo na kuhamasisha.
  • Panga na uandae harambee ili kuchangia mfuko wa umisheni ili kanisa liweze kutoa. Hamasisha utoaji: kila mmoja, kuanzia watoto, anaweza kujifunza kutoa mara kwa mara na kwa moyo. Na pia kumwomba Mungu kuinua watu ili kuwa wamishenari. Kanisa lako liwe linawategemeza wamishenari. Mmishenari atahisi kuungwa mkono na kupendwa.
  • Hakikisha unalea mmishenari au unda kikundi kinachohusika na umisheni.
  • Sisitiza kazi za umisheni katika ibada kanisani kwa kutoa nafasi ya kuelezea kazi za umisheni. Lionyeshe kanisa lako umuhimu wa kujihusisha katika umisheni.
  • Hamasisha kupitia shuhuda na habari za wamishenari na pia sifia historia za maisha yao kwa watu wako. Inapowezekana, tumia vielelezo kama bendera, ramani, picha, uwasilishaji wa kutumia kompyuta na projekta na vijarida.
  • Tengeneza ubao wa matangazo au ukurasa kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya umisheni: bandika ukutani picha za wamishenari wanaosaidiwa na kanisa lako.
  • Jifunzeni kitabu cha Matendo ya Mitume: kihubiri kitabu hiki na uandae somo kwa kina kutoka katika kitabu hiki. Lisaidie kanisa lako kujifunza jinsi kitabau hicho kinavyosema kuhusu umisheni.

Imechukuliwa kutoka Let’s Go! (Mafunzo ya Maingiliano ya Wamishenari) yaliyotolewa na SIM Kimataifa, katika toleo la Aprili 2015.

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us