fbpx Skip to content

Ungependa kujiunga na umisheni – lakini nini kinafuata?

Timu ya AfriTwende imeweka pamoja orodha ya rasilimali ambazo zitasaidia kufahamu nini maana ya umisheni, jinsi ya kujihusisha, na namna ya kuleta watu pamoja nawe katika mpango mkuu wa Mungu wa baraka kwa ulimwengu! Kila kozi inafundisha mpango wa Mungu wa kuleta watu kwake. Kila mmoja unakuonyesha ni kwa namna gani, kupitia maandiko, Mungu ameweka kusudi kwenye taifa la Israeli na kanisa kumjua yeye, pendo lake na kushirikisha wengine neema ya wokovu wake. Lakini ipi ni sahihi kwako? Inategemea na hali yako na kule unakoelekea.

KOZI ZILIZOFUNDISHWA NA MWEZESHAJI ALIYEPATA MAFUNZO

Kozi zifuatazo zinakamata falsafa ya Perspectives na zinapatikana kupitia uhamasishaji rahisi kabisa www.simplymobilizing.com . Baada ya kuhudhuria ndipo unaweza kufunzwa kuwa mwezeshaji.

Perspectives

Kwanza, hebu tukutane na babu wa mafunzo ya Umisheni – Perspectives. Hii ni kozi ya majuma 15 ambayo inahitaji mwezeshaji aliyepata mafunzo pamoja na masaa zaidi ya 50 ya darasani na kazi za kufanya nyumbani. Mafunzo haya yamehakikishwa kuwa yataleta kiwango kipya cha ufahamu wa mamlaka ya kibiblia katika kupeleka ujumbe wa Mungu kwa mataifa. Imebuniwa kwa mitazamo minne: Kibiblia, kihistoria, kiutamaduni na kimkakati. www.perspectives.org

Kairos

Kila mkristo anapaswa kuchukua kozi ya KAIROS, hata kama tayari wana maono kwa ajili ya kuufikia ulimwengu. Kama ilivyowasilishwa na viongozi waliopata mafunzo, vipindi tisa vya kairos vinavyosisimua ni pamoja na video, makundi madogo ya majadiliano na kazi za nyumbani. “Kairos imefungua macho yangu. Moja ya vipindi kilikuwa kinahusu wakristo wa majina tu, na wale waliojitolea. Kupitia kairos, nimejifunza kwamba umisheni ni kiini cha Ukristo. Moyo wangu uwe kwa ajili ya umisheni kama moyo wa Kristo ulivyo kuwa kwa ajili ya umisheni. Labda sijajitoa kama ambavyo nilifikiri kama sijajitoa kwa moyo wa ukristo, ambao ni umisheni. Hii imenipa changamoto ya kuomba, siyo kwa ajili yangu na wale wanaonizunguka, bali pia kwa ajili ya mataifa,” anasema Sarah. (Sarah ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika fani ya udaktari wa familia.)

Youth KAIROS [Vijana wa KAIROS] Hii ni kwa ajili ya vijana wenye umri kati ya miaka 16 na 20. Kozi hii huwasilishwa na mwezeshaji kwa siku tatu na nusu. Inahifadhi maono na uvuvio wa kozi ya KAIROS. www.facebook.com/youthkairos

The Unfinished Story [Hadithi isiyokamilifu] Kama Kairos, TUS inafuatilia mapana ya kazi ya umisheni wa Mungu kutoka kitabu cha Mwanzo hadi vitabu vya Injili, na kwa muda wa miaka 2000 ya vuguvugu la kikristo ulimwenguni. Makanisa ya mahali yanaweza kuitumia kama vile shule ya Jumapili au darasa la kujifunza Biblia. Kuwa kiongozi wa TUS unahitaji kuhudhuria darasani na kuwa na saa chache za mafunzo. TUS inaunda mtazamo wetu wa ulimwengu wa kibiblia ili tuone ushiriki wetu pamoja na Mungu katika huduma kama hali ya kusisimua na ya maana katika kumfuata Yesu!

Empowered to Influence [Kuwezeshwa Kushawishi] Kozi hii ya vipindi vinne imewezeshwa kwa kutumia video ya mfanyabiashara wa Singapore anayeitwa Ken Chua. Mafundisho yake yamejikita kwenye njia mpya saba za kufikiri zinazohitajika ili waumini kuwa washawishi kwa ajili ya Mungu katika maeneo yao ya kazi, kanisani na nyumbani. Ingawa inafaa zaidi kwa wafanyabiashara, lakini itamwezesha kila mwamini kuzitumia.

Interface [Mwingiliano] Kozi ya “Interface” kinajibu swali hili: “je, kanisa lililojiunga na umisheni pamoja na Mungu linaonekanaje?” Utangulizi wa uwasilishi unafuatwa na semina ya siku moja au warsha ndefu. Inavumbua muundo wa kanisa ambao utalea, utaandaa na kuruhusu watu wa Mungu katika huduma inayoleta mazao.

 

Kwa taarifa zaidi kuhusu lini na wapi unaweza kupata kozi hizi, wasiliana na: Afrika Mashariki: samuangugi@gmail.com

MASOMO YA BURE AMBAYO YANAPAKULIKA KUTOKA KWENYE MTANDAO NA UNAWEZA KUJIFUNZIA NYUMBANI

XPLORE Masomo haya saba ya kundi dogo la kujifunza yanawakilisha taarifa ya sasa juu ya hali ya Ukristo ulimwenguni, sambamba na makundi ya watu ambayo bado hayajafikiwa na Injili ya Kristo pamoja na dini nyingine kubwa. Kinafundisha tabia tano ambazo waumini wote wanaweza kuziweka katika matendo na kubadilika kuwa wakristo wa ulimwengu. www.mobilization.org/resources/live-missionally/xplore/

Go Mobilize [Nenda Uhamasishe] Hatua hii nyingine inafundisha kile kinachotakiwa kwa mtu ambaye ni mhamasishaji na jinsi ya kuanza vuguvugu la umisheni miongoni mwa rafiki zake na mawasiliano yake. Masomo haya ni pamoja na namna ya kutumia maandiko kuwaonyesha wengine shauku ya Mungu kwa kila taifa, na jinsi ya kuwaelekeza wengine mahali ambapo bado hakuna injili au uwezekano wa kuingia ni mdogo. www.mobilization.org/resources/mobilize-others/go-mobilize/

Your Church Can Change the World [Kanisa lako laweza kubadilisha dunia] Kitabu hiki cha mafunzo ambacho hutolewa bure kinaweza kuboreshwa kulingana na muktadha wako. Kimeandikwa nchini Mexico na kimekusudiwa kwa ajili ya wakristo waliokomaa kiimani, na baadhi ya sehemu za kitabu hicho zinaeleza “Kwa nini Kanisa Linapaswa kujihusisha na umisheni, kuomba kwa ajili ya ulimwengu, mahitaji ya fedha kwa ajili ya kazi za umisheni na kamati za umisheni katika Kanisa la Mahali. www.yourchurchcanchangetheworld.org/

Kama una shauku kuhusu umisheni na unataka kuona wengine wakitambua uwezo wao wa kwenda, kuomba au kutegemeza kifedha, basi unaweza kuwa mhamasishaji. Shirikiana na mashirika yaliyoko katika eneo lako au uwasiliane na simplymobilizing: https://simplymobilizing.com/mobilizers/

NYENZO/VIFAA VYA MAFUNZO

 Sehemu ya kuhamasisha ni mafunzo kwenda nje au kutumika pale ulipo. Vifaa vingi vinapatikana, ingawa wengi wanahitaji kujisajili kwenye program. Hapa kuna rasilimali chache za bure ambazo unaweza kutumia katika muktadha wako.

Go-er Groups [Makundi ya Wanaotaka Kwenda] Somo hili hutolewa bure kwa mfululizo wa vipindi saba kwa njia ya video kwa wanafunzi walioko kwenye maeneo ya mijini. Somo hili linaibua maswali makuu na vikwazo ambavyo wakristo wanakumbana navyo wanapokuwa wanafanya huduma katika tamaduni tofauti tofauti. Video hizi zenye mtiririko wa masomo zina ushauri mzuri kutoka kwa watu wenye uzoefu. Zitumie kufanyia kazi masuala ya msingi wakati ukifikiria kuwa mmishonari. www.mobilization.org/resources/prepare-for-ministry/

Crossing Cultures [Kuvuka Mipaka ya Utamaduni] Waamimi wengi hutamani kuwafikia watu katika jamii zao ambazo zina tamaduni au dini tofauti lakini wanakuwa waoga kutokana na kukosa uzoefu, maarifa au stadi. Warsha hii ina shughuli za kufurahisha na za kuwaandaa watu ili waweze kuwasiliana na watu katika tamaduni zingine – stadi inafaa nyumbani na mahali pote duniani. Mshirika wa kanisa anaweza kuongoza kazi hii baada ya muda mfupi tu wa mafunzo. www.simplymobilizing.com/courses/crossing-cultures/

Encountering the World of Islam [Kukabiliana na Ulimwengu wa Uislamu] Watu wengi ambao bado hawajafikiwa na Injili ya Yesu Kristo ni Waislamu, na bado Wakristo wengi wanafahamu kidogo sana kuhusu historia au imani za dini ya kiislamu. EWI ni kozi iliyowezeshwa ambayo inaweza kukupa mwanga na maarifa katika ulimwengu wenye migongano, na kujua habari za zamani zinazohusu miungu ya Kiislamu. Utajifunza namna ya kuwaombea, kuanzisha mahusiano nao, na namna ya kuwafikia Waislamu walio karibu nawe. Madarasa yapo nchini Ethiopia, Kenya, Nigeria, Afrika Kusini na Rwanda. info@ewi.org www.encounteringislam.org

Let’s Go! [Twendeni] Kitabu cha shirika la SIM kisemacho “Na Twende!” ni kitabu kinachosadia kufahamu namna ya kuanza mahusiano na mtu, ingawa hakichukui nafasi ya mafunzo rasmi, lakini ni kitabu kinachotoa mafunzo kwa vitendo, kufanya mafunzo yawe na maana zaidi kwa mtumiaji. Kuna simulizi na shuhuda, vipeperushi, makala, Biblia za kujifunzia, na video fupi za kihabari zimetengenezwa ili ziweze kusomwa pamoja na mshauri/mwelekezi kwa muda wa miezi sita mpaka 12. Zinaweza kupatikana kwenye mtandao: bit.ly/LetsGOpdf – PDF version bit.ly/LetsGOsupplemental – supplemental material bit.ly/LetsGoVideos – videos for the chapter.

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us