Unaweza kuwafikia Waislamu: rasilimali za kukusaidia
Je unataka kuwafikia Waislamu wanaokuzunguka, lakini unaanzaje? Timu ya AfriTWENDE imetayarisha vitabu, kozi, na video vya kukusaidia.
Shirika la Life Challenge Afrika (LCA) lina aina mbalimbali za vitabu kwenye tovuti yao. Vingi vya vitabu hivi vinapatikana kama PDFs na bei zake ni ndogo. LCA ina PDFs za mada za aina mbalimbali ambazo zinaweza kukusaidia kufahamu Uislamu na Waislamu. https://www.life-challenge.org/resources/ LCA imeturuhusu kwa uzuri kabisa kutumia baadhi ya rasilimali zao kwenye kurasa ya tovuti yetu, ili uweze kupakua bila malipo. Tembelea uone kilichopo kutoka AfriTWENDE. https://afrigo.org/islam-resources-swahili/
VITABU:
Mambo yaliyosabisha Maendeleo ya Uislamu
Kipeperushi hiki kinaongelea pale Uislamu kikielezea kwa kifupi chimbuko, muanzilishi na kwa namna ipi Uislamu uliendelezwa. Lakini pia kinaelezea uislamu na baadhi ya maneno muhimu na maana zake katika dini hii.
https://afrigo.org/wp-content/uploads/2024/04/Mambo-yaliyosabisha-Maendeleo-ya-Uislamu.pdf
Nani Anakwenda MbinguniHuu ni ushuhuda mfupi wa Isaka kuhusiana na mtu aliyesahihi
kwenda mbinguni na atakaye kwenda jehanamu. umegusia
safari yake ya familia ya uislamu mpaka pale alipompokea
Kristo na maisha yake akiwa anamtumikia Mungu.
https://afrigo.org/wp-content/uploads/2024/06/Nani-anakwenda-Mbinguni.pdf
Uislamu na Waislamu
Kitabu kinaeleza kuhusiana na Uislamu, amri zake, Kurani, na vitu vya kujua kama mkristo kwenye Kurani, uislam ulipoanzia, Mwanzo wa maisha ya mtume Muhamadi kwa undani zaidi kuanzia kuzaliwa kwake, maisha aliyoishi hadi mwisho, pamoja na imani yao juu ya Allah. Lakini pia inaeleza namna tunavyoweza kulinganisha ile Kweli ya Yesu kwa Busara kama mkristo kutokana na Kurani hoja ambazo Waislamu wanajenga kutokana na ukristo na injili na mengineyo mengi kiundani zaidi.
https://afrigo.org/wp-content/uploads/2024/06/Tunyoshe-Mkono-Bk2009.pdf
Mambo Kurani hufundisha kuhusu Biblia
Kitabu hiki kinakupa muangaza kwa kifupi vile Kurani hufundisha waumini wake juu ya Biblia na namna wanavyoitafsiri Biblia. Vitabu hiki kinakupa muangaza kwa kifupi vile Kurani hufundisha waumini wake juu ya Biblia na namna wanavyoitafsiri Biblia.
https://afrigo.org/wp-content/uploads/2024/06/MAMBO-AMBAYO-KURANI-HUFUNDISHA-KUHUSU-BIBLIA.pdf
Habari zako Unazijua
Kitabu hiki kidogo kinaongelea namna habari za mwanadamu zimeanzaa katika msingi mkuu wa Mungu na kuishia na Mungu kuanzia kwenye kuzaliwa na imani ya mwanadamu laana na ahadi ya Mungu kwake hata baada ya kuasi, na sadaka aliyoitoa Mungu kupitia mwana wake pale msalabani. Kama vile maandiko matakatifu yalivyo nukuliwa na kutunzwa bila ya hivyo hakuna ambaye angeweza kujua habari zake na historia yake bila ya Mungu. https://afrigo.org/wp-content/uploads/2024/06/YourStorySwahili.pdf
Umeumbwa kwa Kusudi
Kitabu hiki kinafafanua kusudi la kuumbwa kwako, na safari ya mwanadamu kwa ujumla tangu alipoumbwa na Mungu, ahadi aliyopewa na Mungu, alipoanguka na Msamaha wa milele aliopewa na Mungu.
https://afrigo.org/wp-content/uploads/2024/06/01-Umeumbwa-kwa-Kusud-Swahili.pdf
Shiriki Hii
Mtu Mwenye Ujumbe wa kijitabu hiki kinaweza kupakuliwa bila malipo kwenye tovuti yetu ya https://afrigo.org/ islam-resources-swahili/ na kinaweza sambazwa kwa marafiki waislamu, majirani na wanafamilia. Itumie ikiwa ni zana ya uinjilisti.