fbpx Skip to content

Ujuzi na Stadi: Zana Mikono ya Mungu

Dk. Bode Olanrewaju ni daktari wa mifugo na mmishenari anayefanya kazi na shirika la CAPRO. Anatumia taaluma yake kuwafikia wale walio katika vizuizi wasifikiwe na injili katika sehemu za kaskazini mwa Nigeria.

Ni heshima kubwa kutumia maarifa ya udaktari wa mifugo kuwahudumia watu masikini ambao maisha yao yanategemea mifugo. Hii imeniwezesha kuwa mfano wa upendo wa Kristo na huruma katika namna inayoonekana.

Msaada wangu wa utaalamu wa mifugo kwa kabila la Wafulani ni daraja la kuanzisha mazungumzo, ambapo vizuizi vya kutokuaminiana na mtazamo hasi walionao watu juu ya wakristo vinavunjwa. Kila mmoja anaweza kutukaribisha kwa upendo kama tu tunaweza kugusa mioyo yao. Mioyo ya Wafulani inaguswa pale tunapojali makundi yao ya mifugo.

yao ya mifugo. Kila familia kijijini ina kuku. Kiukweli kuku ni kama ‘ATM’ (mashine ya kutolea pesa benki) ya maskini. Lakini magonjwa huangamiza makundi ya kuku na ng’ombe.

Kwa hiyo, tunawafunza wenyeji na wamishenari kuwa sisi tu watoa kinga au chanjo kwa jamii. Hii imetupa upenyo mpana kwenye kaya na imekuza sana kuaminiana. Baadhi ya watu wanadiriki hata kutushirikisha habari za ndani za maisha yao kwa kadiri wanavyoona upendo wa Kristo katika maisha yetu.

Shuhuda kama vile, ‘nilipata ada ya shule ya watoto wangu kwa kuuza kuku wa kienyeji’, zipo nyingi miongoni mwa wale wanaonufaika na mpango wa mfuko wa shirika la Tearfund kutoka Uingereza, ambalo ni mshirika wetu wa muda mrefu. Uboreshaji wa uzalishaji wa kuku wa kienyeji umekuwa na matokeo mazuri katika kuboresha maisha ya watu.

Muislamu ambaye alikuwa amekataa hata kumsalimia mmishenari mzalendo alibadilisha mtazamo wake pale alipoona kuku wake wamechanjwa na mmishenari na hawakuweza kufa pale magonjwa ya mlipuko yalipotokea. Alikuja na kutuomba tukachanje makundi ya mifugo yake!

Leo madaktari wa mifugo, madaktari wa binadamu, wataalamu wa mifumo ya kompyuta na wengineo wanahitajika sana kutumia stadi zao kusaidia wapanda makanisa na kutoa nafuu za maisha kwa jamii zilizopigwa na umaskini. Hata kujihusisha na kazi za umisheni kwa muda mfupi kunaweza kuleta tofauti kubwa.

Jane Banda, Kocha wa mchezo wa pete, hufanya kazi na Sports Friends (Marafiki wa Michezo), ni huduma chini ya SIM inayotumia michezo kama zana kwa ajili ya kubadilisha maisha kupitia injili. Jane anatoka Malawi, ambapo Wakristo wengi hawakuwa na ndoto ya kutumia michezo kama zana ya huduma ya kupeleka injili.

Siku moja Marafiki wa Michezo walioko Malawi walitambulishwa kwenye kanisa la Jane. Alikuwa ameacha kucheza mpira wa pete kwasababu ya kutoelewana na wazazi wake. Wazazi waliamini kuwa kumruhusu msichana kushiriki katika michezo ni kumpoteza na kujiingiza katika ukahaba.

Marafiki wa Michezo wa Malawi waliwapa wazazi wake habari mpya, na ndipo wazazi wa Jane walipoamua kumwacha Jane ashiriki katika michezo. Sasa Jane ni mmoja wa walimu wa kutumainiwa wa mpira wa pete na anaongoza timu ya mpira ya kanisa lake.

Watoto wengi wanampenda Jane na huduma yake ya michezo. Baadhi ya watoto anaowafundisha wamemwamini Yesu na sasa ni sehemu ya kanisa. Wazazi wake Jane wanafurahi kwa sababu Jane anaendelea kuifikia jamii kwa ajili ya Kristo.

Hadithi ya Jane inamkumbusha andiko lisemalo: ‘Jiwe lililokataliwa na mjenzi siku moja lilikuwa jiwe kuu la pembeni’. Michezo ambayo ilidhaniwa kuwa ni kitu kibaya na kingeleta tabia mbaya, bali sasa ni zana kubwa ya kubadilisha maisha! Ni kweli Jane anajishughulisha na kazi za kanisa na kuigusa familia yake. Pia ana furaha ya kuwaona wanajamii wakimwamini Kristo.

2.1 Rev Fussi

Mch. Edwin Fussi ni mmishenari mwenye historia ya kuwa mfanyabiashara; aliimiliki duka dogo kabla ya kusoma shule ya umishenari na kuanza kazi ya umisheni katika makundi ambayo bado hayajafikiwa na injili nchini Tanzania.

“Familia yangu ilipofika katika jamii ambayo tunatumika sasa, asilimia 99.9 walikuwa ni Waislamu. Kulikuwa na vikwazo vingi dhidi ya injili. Tulikataliwa, tulitukanwa na kudhihakiwa. Nilitambulishwa kwa wanakijiji kama mchungaji, mwalimu na kiongozi wa dini ya kikristo. Mkakati wetu ulikuwa wa uinjilisti wa nyumba kwa nyumba, lakini jamii ilitukataa.

Vijana walitukimbia walipotuona wakidhani sisi ni wapelelezi wa serikali. Viongozi wa misikiti waliwazuia watu wasichangamane na sisi ili wasiwe Wakristo. Baadhi ya watu walituambia kuwa ‘sisi tuna dini yetu na wao wana dini yao.’ Tulimwomba na kumsubiri Bwana. Kulikuwa na changamoto ya makanisa yaliyotutuma kupunguza msaada wa kipesa baada ya kuona hakuna matokeo na watu kujiondoa kwenye kikundi cha waombaji. Nilianza kufikiri kuwa ingekuwa vema kama ningeiacha kazi hii—maana ningerudi nyumbani na kuendelea kuhubiri injili na huku nikiendelea na biashara zangu.

Lakini siku moja nilipokuwa nasoma Biblia, Mungu alinionyesha jinsi Mtume Paulo alivyoweza kutumia ujuzi wake katika huduma. Bwana aliniambia, “unaweza kuendelea kunitumikia katika kijiji hiki na kushinda changamoto kama tu utatii na kutumia ujuzi niliokupa.” Nilisema, “asante Bwana. Najua jinsi ya kuendesha biashara. Je, inawezekana kuanza biashara hapa na huku nikiendelea na malengo ya kuwafikia watu kwa injili?”

Kwa mtaji mdogo, nilianzisha duka dogo la kuuza vifaa vya umeme wa jua na vinywaji. Nilikuwa nachaji simu za mkononi na betri pamoja na biashara ya kunyoa nywele. Baada ya miezi michache niliweza kutengeneza marafiki wengi. Wanakijiji waliacha kutufikiria sisi kama maadui. Hapakuwa na umeme katika kijiji chetu kwa wakati huo, lakini waliweza kuchaji simu zao na kununua vifaa vya umeme wa jua na kunitaka mimi niwawekee mfumo wa umeme. Niliweka mistari ya Maandiko katika taa zote nilizowafungia. Uendeshaji wa biashara uliondoa vikwazo vingi vilivyokuwepo, na ilitusaidia kujenga daraja imara la kuyafikia makabila katika eneo hilo.

Msanifu wa Majengo, Tito Oludotun Kumapayi ni mkurugenzi wa shirika la Umisheni na Uinjilisti kwa makanisa ya Nigeria, Usharika wa Kianglikana. Ana ofisi ya usanifu majengo katika mji wa Ibadani, mahali ambapo anaishi na mke wake, Margaret.

Mwaka 1991, nikiwa katika chuo cha Hagai huko Singapore, nilishawishika kuwa nisiwekwe wakfu kuwa mchungaji bali niendelee na kazi yangu ya Usanifu Majengo na niitumie kwa ajili ya uinjilisti, kuleta roho kwa Kristo na kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu.

Kwa hiyo, katika ofisi yangu, kila siku nilianza na maombi na kusoma Biblia kwa muda wa dakika kama 30 hivi. Kwa kadiri ushirika huo ulivyoendelea kukua, baadhi ya wafanyakazi walikuja kwangu na kutafuta ushauri kuhusu masuala ya kazi na ndoa. Baada ya muda mfupi ushirika wetu ulianza kusafisha wafanyakazi wetu kwa maana ya kujitoa zaidi kufanya kazi na kusimamia miradi. Ofisi yetu ilianza kuvutia wakristo waliotaka miradi yao ifanywe vizuri.

Wakati mmoja tulipokuwa tunasimamia mradi wa serikali, mmoja wa wajenzi wetu ambaye ni muislamu mmoja alikuja na kusifia kazi na jinsi kazi yetu ilivyokuwa inakwenda vizuri. Baadaye alikuja kwangu na kuamua kutoa maisha yake kwa Kristo. Muislamu huyu aliyebadilika na sasa anatumika kama Shemasi katika kanisa la mtaani kwao.

Kama ambavyo madhabahu ni kwa mtumishi aliyewekwa wakfu, ndivyo ilivyo mahali pa kazi kwa mkristo mwenye taaluma. Mtu mwenye taaluma anaweza kupakwa mafuta kuhudumu katika mazingira yake kwa ajili ya ukuaji wa ufalme wa Yesu Kristo. Mara kadhaa nawaambia watu kwamba kazi halisi ni kuleta roho kwa Kristo na kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu, ilhali kazi ya usanifu majengo ni ya muda tu.

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us