fbpx Skip to content

Neno ambalo halitarudi bure

Akiwa na umri wa miaka 12, mvulana wa kisomali, alikuwa tayari alishajifunza Kurani yote. Aliweka kwenye kumbukumbu sehemu za Kurani kwa Kiarabu, lugha ambayo hata alikuwa hajui maana yake. Alipofikia umri wa miaka 18, alikwenda kuishi na mjomba wake katika Jiji la Mogadishu. Siku moja alikuta kitabu kwenye kabati la kuwekea vitabu, chenye jina ‘ Bibilia Takatifu.’ Akifikria kuwa ni Koran iliyotafsiriwa kwa Kisomali, alianza kuisoma. Katika hali ya mshangao, aligundua kuwa kitabu hicho cha Biblia, kilikuwa kinahusu imani tofauti na kwamba mjomba wake alikuwa mfuasi wa Yesu Kristo. Alimwomba Allah amsamehe kwa kugusa na ‘kitabu cha makafiri.’ Lakini kitu fulani kilimvuta.

‘‘Niliendelea kukisoma,’’ anasema. ‘’Nilihisi kuwa hili lilikuwa ndilo Neno la Mungu lililokamilika na la kwanza. Kadiri nilivyosoma Agano Jipya, haiba na ujumbe wa Yesu Kristo viligusa moyo wangu. Kama mwislamu, namwabudu Allah kwa njia ya kuogopa, lakini kupitia kwa Yesu, Mungu ni baba yangu ambaye ananipenda zaidi ya anavyonipenda baba yangu mzazi.’’

Baada ya miaka miwili ya usomaji wa Biblia, Mungu alimwondolea hofu zote na Abdi alimwamini Yesu kwa ukamilifu wote kama ‘njia, kweli na uzima’ (Yohana 14:6). Hatimaye, alipata ujasiri wa kumwomba mjomba wake kwenda naye kanisani. Alijiunga na ushirika mdogo la kiprotestanti wa watu kama 20 hivi katika mji wa Mogadishu, ambapo alifundishwa kuwa mwanafunzi na kubatizwa mwaka 1989.

Miaka 30 baadaye Abdi Duale na mke wake Kawser Omar ni wamishenari wanaofanya kazi pamoja na SIM, wakiwafikia Wasomali kwa injili duniani kote, wakitumia njia mbalimbali kupitia majukwaa ya mtandaoni.

KUTAZAMA NYUMA

Kuna usemi kwamba, ‘’kuwa msomali ni kuwa mwislamu.’’ Uislamu ulifika karne ya 8 nchini Somalia, na leo hii wasomali karibu wote wanaishi maisha ya Uislamu wa Sunni. Misheni za Kikristo zilianza kwenye miaka ya 1880 lakini zilikumbana na changamoto nyingi. Biblia nzima inapatikana kwa lugha ya kisomali, lakini ni asilimia chini ya moja tu ya wasomali wote ni wakristo. Wasomali wameridhika na Uislamu na wanaona unajitosheleza, huku wakipinga na kutumia nguvu ya upinzani wa kijamii kwa wale wanaothubutu kumfuata Kristo.

Vita vya wao kwa wao nchini Somalia vilivyo anza mwaka 1987 hadi 1991 na viliifanya Somalia itangazwe kuwa ni “nchi iliyoanguka kiutawala.” Wakristo wengi waliuawa, ikiwa ni pamoja na mjomba wake Abdi. Sehemu ya Somalia iliyojulikana kama Somaliland ilijimega na kujitenga na hivyo kwa sehemu kubwa imebaki na amani wakati Somalia imeendelea kuteseka kwa vurugu na njaa. Theluthi moja ya nchi inadhibitiwa na kundi la kigaidi la Al-shabaab. Vita pia imefanya Wasomalia wengi kuikimbia nchi na kwenda uhamishoni katika sehemu mbalimbali za dunia.

VYOMBO VYA HABARI VYA MAISHA MAPYA

picha na AIM Stories

Kama ambavyo Abdi aliweza kupata kitabu kwenye shelfu ya vitabu vya mjomba wake, huduma ya vyombo vya habari vya maisha mapya inatoa fursa kwa wasomali kutafuta Biblia pale wanapongalia tovuti na mitandao ya kijamii.

Huduma hii ilianza mwaka 1972 kama sauti ya matangazo ya Redio ya masafa mafupi ya Maisha Mapya na iliendelea kupanuka na mwaka 2006 ilianza kupatikana kwenye tovuti na mwaka 2014 ilianza kupatikana kwenye Facebook na YouTube. Majukwaa haya huwapa watu nafasi kujua ukweli wa Mungu wakiwa kwenye usiri majumbani kwao. Kwa hiyo, Wakristo wanaweza kufanya ushuhudiaji kwa ujasiri bila hatari inayoweza kutokana na kuhubiri injili hadharani.

Maudhui ya mtandaoni yanajumuisha aina nyingi za Biblia, pamoja na viwezeshi vya kompyuta kama URLS, zinazomsaidia msomaji kutafuta sura na mistari ya Biblia kwa urahisi. Miziki ya Kikristo kwa Kisomali pia inawekwa kwenye mitandao hii ya kijamii. Video ya hivi karibuni mtandaoni ya wimbo kuhusu mateso wa Kan ii dudayaa yeelkii (Sijali juu ya yule anayeniudhi) ilipata watazamaji zaidi 210,000.

Mfuatano wa video unaoitwa Neno la Mungu na methali za kisomali zilizowekwa kwenye mtandao hivi karibuni ambayo ilikuwa na hoja zinazopinga mtazamo kuwa ni vigumu kubadilika, ilitazamwa na watu zaidi ya milioni moja. Mjumuiko wa hadhira ni wa juu, na lengo la maudhui ni kufikia mawasiliano ya uso kwa uso pamoja kwa minajili ya kujifunza zaidi.

Abdi anasema kwamba kwa wale wanaomfuata Yesu, wengi wao inawachukua miaka mingi kuweza kumwambia mtu kuhusu habari za Yesu, wakiweza. Anaongeza Abdi, ‘’ wamekuwa mateka wa utamaduni.’ Abdi na mkewe Kawser wanakabiliwa na vitisho ambavyo Abdi anaviita kuwa ni vya ”kawaida’’. Haya yanakuja kama maoni kupitia video zinazowekwa kwenye mitandao ya kijamii. Familia yao imepuuza vitisho hivyo tangu walipogeukia imani ya kiKristo miongo kadhaa iliyopita.

RUNINGA YA INJILI YA SOMALIA

Mwaka 2020 Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, aliitisha siku ya kitaifa ya maombi. Abdi na mkewe Kawser walialikwa kuwasilisha kipindi kwa lugha ya kisomali ambacho kilirushwa kwenye Runinga ya kitaifa inayoonekana nchini kote Mei 10, 2020. Kipindi cha pili cha ibada kilirushwa mwezi Juni 2021. Mkurugenzi wa New Life Media, Michael Madany, alisema, ‘’ Kwa kadiri tunavyojua, hii ni mara ya kwanza kwa kipindi cha kikristo katika lugha ya kisomali kutangazwa na runinga ya taifa.’’’ Kwa kadiri tunavyojua, hii ni mara ya kwanza kwa kipindi cha kikristo katika lugha ya kisomali kutangazwa na runinga ya taifa.’’

Tangu wakati huo, kupitia ushirika na shirika la kimisheni la SIM, na la Kuhubiri Injili katika pembe ya Afrika (The Horn of Africa Evangelical Mission), vipindi zaidi vimeandaliwa kwa ajili ya kutangazwa kupitia runinga ya Setelaiti ya shirika la Uinjilisti la Ethiopia. Ni kupitia njia hii ndipo Runinga ya Injili ya kisomali ilizaliwa mwaka 2021.

Pamoja na vikwazo vikubwa vya kiasili dhidi ya uinjilisti na upandaji wa makanisa miongoni mwa wasomali, njia mpya za kidijitali zinabeba neno lililo hai la Mungu kwenda kwenye nyumba na mioyo ya watu ambao BWANA wetu hajawasahau. Washuhudiaji waaminifu kama Abdi, mkewe Kawser na timu yao wanahatarisha maisha kwa kuamini kuwa Neno litatimiza kile ambacho Mungu anapendezwa nacho na litafanikiwa kwa kile lililotumwa kufanya (Isaya 55:11).

JIFUNZE ZAIDI

Somali worship service on Ethiopian TV: https://bit.ly/Somaliworship

Somali Gospel TV – Facebook: https://bit.ly/3NJ31C5

Somali Gospel TV – YouTube: https://bit.ly/3NMwBXa

New Life website: https://noloshacusub.com/

TAFADHALI OMBA KWA AJILI YA:

  • Kwa Wakristo waweze kuomba na kuwafikia Wasomali walio nje ya nchi yao.
  • Ulinzi kwa waumini na wafanyakazi wa huduma.
  • Maarifa ya kupambanua roho wanapokutana na ngome za giza.
  • Kumshukuru Mungu kwa ajili ya watu wanaojifunza kupitia mitandao na watenda kazi wa huduma ya Mungu Mmoja, Njia Moja.
  • Wote wanaohusika na kazi hiyo.

Ushuhuda wa Msomali

’Nawasalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kupitia yeye nimepata wokovu, neema na uzima wa milele. Kwangu kuwa mkristo kumeniletea shida nyingi. Mke wangu na watoto wetu watano walianiacha pale niliposema siwezi kuikana imani yangu katika Kristo. Nilihukumiwa kwenda jela kwa miezi 20, lakini niliachiliwa baada ya miezi sita tu. Hakuna mtu aliyenifanya mimi kuwa mkristo; hiyo ilikuwa ni kazi ya Mungu. Sijawahi kumwona mkristo mwingine; hata hivyo, nimepakua Biblia ya kisomali kwenye simu yangu. Sijasoma sana, na nafanya kazi kama kibarua. Nimekuwa mkristo kwa miaka sita sasa na bado ni mchanga katika kutumia mitandao ya kijamii kama Facebook. Simu yangu ya mkononi ya kwanza ilikuwa ndogo sana; angalau ilikuwa na Google na kwa hiyo niliweza kupakua Biblia. Nimeisoma karibu yote kutoka Mwanzo hadi Ufunuo. Namshukuru BWANA ambaye alinikomboa kutoka gizani, kwenye ujinga na kivuli cha mauti. Natembelea kila tovuti ya kisomali inayotangaza Injili ya Mungu.”

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us