Mhamasishaji Mzoefu Ashirikisha Ufahamu Wake
By Mercy Kambura
Kehinde Ojo alikuwa miongoni mwa wanafunzi bora wa chuo kikuu alichosoma, akisomea uhandisi wa umeme na elekroniki. Pia alichaguliwa kuwa sehemu ya menejimenti, akijifunza kazi za uongozi katika moja ya makampuni makubwa ya mafuta yaliyokuwa yanalipa vizuri sana nchini Nigeria.
Akiwa mtu anayejifunza kazi za kiwandani, aliahidiwa kazi katika kampuni hiyo, kazi ilioangazwa taaluma yake ya maisha bora ya uhakika. Lakini baada ya kumaliza mafunzo, Ojo hakurudi. Miaka miwili baadaye aliwatembelea marafiki zake waliokuwa wamepata kazi. Walishangaa sana! Ni nani mwenye akilli timamu angeweza kuachia fursa kama hiyo ipotee? Ojo aliwatangazia wale wenzake kwa kusema: “Nimepata kazi bora zaidi.”
Kehinde alikubali wito wa kumtumikia Mungu katika Ushirika wa Kimataifa wa Wanafunzi wa Makanisa ya Kiinjili (International Fellowship of Evangelical Students-IFES). Nafasi yake ilikuwa kuwafanya wanachuo kujua masuala ya Uanafunzi, na uhamasishaji kuhusu umisheni miongoni mwa wanafunzi waliokuwa wanaishi vyuoni.
Leo Kehinde ni mkufunzi, mtaalamu, na mshauri. Baada ya miaka 20 akiwa na IFES Nigeria, Kehinde alialikwa na IFES kuanzisha mpango mpya wa kiulimwengu kusaidia vuguvugu za kitaifa ndani ya IFES ili iweze kujitegemea kupitia harambee za kuchangisha fedha na kuifanya iweze kuwa na matokeo mazuri. Katika kuandaa mpango wa kazi, Kehinde alitengeneza timu ya kimataifa kufanya kazi naye. Anafundisha na kuandaa viongozi Afrika, Ulaya-Asia, Caribbean, Marekani ya Kusini, Asia ya Mashariki na kanda za kusini mwa Asia. IFES imetoa msaada kwa mashirika mengine katika sehemu mbalimbali za ulimwengu katika jitihada zao za kutaka kujitegemea.
Akiwa na timu ya wakufunzi 15 kutoka sehemu mbalimbali duniani, Kehinde huendesha mafunzo katika nchi kadhaa kila mwaka. Hakuna kona ya ulimwengu ambayo haijulikani kwake, baadhi ya sehemu hizo ni kama Fiji, Vanuatu, Guyana, Jamaica, Nepal, na Gambia.
Mikakati Mitatu
Ili kuwa na uhamasishaji wenye matokeo mazuri, Kehinde anashauri mikakati mitatu mikuu kwa mhamasishaji:
- Uthibitisho/Uhalisi furaha
“Mkakati wenye matokeo kwa mhamasishaji yeyote unapaswa kuwa na uthibitisho wa ukweli,” anasema, Kehinde. Hili ni jambo moja ambalo linaleta mafanikio kila wakati. Kama mhamasishaji, watu wanataka uwe mkweli. Kizazi cha vijana kinataka kukuona wewe unaishi maisha halisi na unatumia kanuni zile ambazo unawasihi wao wazifuate.”
- Uthabiti/ Kutobadilika
“Ishi kwa kufuata kanuni unazofundisha na shikilia maono uliyonayo. Maandiko hayapitwi na wakati. Uendelee na kweli zako za kibiblia na kuwaonyesha watu wito usiobadilika katika umisheni.”
- Usiagize matendo, uliza maswali
“Njia inayooonekana kana kwamba ni bora ya kuwajulisha watu maono yako ni kwa kusimulia maisha yako. Hata hivyo, huenda watu wasitambue uzoefu wako na wanaweza kukosa kuona jinsi wanavyoweza kuchangia katika maono yako. Badala yake, waache watu wajihusishe kutokana na hali halisi waliyonayo- kwa namna inavyoweza kufaa kwao. Hili likiwa katika akili zao, wanaweza kutoa jibu.
Nje ya Chuo Kikuu
Kehinde alikulia kusini magharibi mwa Nigeria. Licha ya kuzaliwa katika familia ya kikristo na kubatizwa siku ya nane tu baada ya kuzaliwa, aliyatoa maisha yake kwa Krsito alipokuwa Chuo Kikuu. Haikuwa ni wokovu tu alioupata katika miaka hii akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu, bali pia alipata wito wa maisha yake. Hii ilitokea juma moja tu kabla ya kufanya mtihani wake wa mwisho.
“Sikuwa na raha Jumapili hiyo, niliacha hata ibada nikaenda kuomba peke yangu kwenye bustani.” Alihisi kwamba mwelekeo wa maisha yake ulikuwa kwenye ukingo wa kubadilika, lakini hakuweza hata kuelewa. Wakati wa ibada, Mungu alizungumza kupitia mhubiri kwamba miongoni mwa wahitimu wa Chuo Kikuu, Mungu alikuwa anamwita mmoja wao kumtumikia.
“Ni mimi tu nilitokea mbele siku hiyo; hapakuwa na kuchanganyikiwa hata kidogo,” anaongeza. Miaka 31 baadaye, chaguzi za maisha yake yote zimechongwa na uamuzi huo mmoja.
Rasilimali Tatu
Kwa muda wa miaka tisa iliyopita, jukumu la Kehinde limekuwa ni kuhamasisha na kuandaa harakati ya kitaifa ya IFES kukubali manufaa ya kujitegemea kwa kutumia rasilimali ziliziko katika mazingira yao. Hii hufanyika kupitia tafiti, mafunzo, ushauri/ufundishaji, na kupanga ruzuku zinazoendana. Kama mhamasishaji, Kehinde husisitiza rasilimali tatu ambazo wakristo wanaweza kuzitumia kupeleka injili mbele.
- Muda
Kitu kinachomsawazisha kila mtu ni muda! Sote tuna muda ulio sawa. Ni kwa jinsi gani washirika ambao hawana fedha au stadi wanaweza kutumia muda wao kutumikia huduma? Kimsingi wanaweza kutumia sehemu ya muda wao kuomba kwa ajili ya umisheni na kutembelea washirika katika umisheni.
- Talanta
Wengine wana stadi na wana uwezo mkubwa katika taaluma zao. Watu hawa wanaweza kujitolea kufanya kazi kwenye huduma na kutoa huduma ambayo isingepatikana bila kulipiwa.
- Hazina
Aina ya hazina inaweza isiwe na muda au kipawa kuwepo, lakini wanaweza kutoa rasilimali kama pesa au vitu ambavyo vinaweza kusaidia mahitaji ya shirika. “Rasilimali za muda, talanta, na hazina ziko kila mahali! Kwa miaka mingi, viongozi wengi wa huduma wamejielekeza kwenye uhamasishaji wa pesa, huku wakiacha rasilimali zingine. Viongozi wanahitaji kufungua rasilimali hizi zingine ambazo zinapatikana katika mazingira yao na kuziachilia kwa ajili ya maendeleo ya huduma,” anasema Kehinde.
Je, kwa miaka 29 baadaye, Kehinde amejuta uamuzi wa kujiunga na uanafunzi na uhamasishaji wa shughuli hii? La, hasha!
“Sijawahi kuacha kutumia maarifa yangu ya uhandisi na stadi hata katika kazi yangu ya sasa; bado natumia kanuni za uhandisi kufanya maamuzi”. Maneno katika 1 Nyakati 29: 1 yameendelea kuwa faraja kwangu. Mfalme Daudi aliuambia mkutano: “Mwanangu Sulemani, ambaye Mungu pekee aliyemchagua, ni kijana mdogo na asiye na uzoefu; na kazi ni kubwa.” www.ifesworld.org