Makundi Ya Watu:Wadatooga
Wadatooga ni jina la ujumla kwa makundi ya Jamii moja ya wafugaji wnaohama yenye asili ya Nilotiki, ambao ni Wabarabaig, Wataturu, Rotigenga, Gidang’udiga, Simijiega, Burediga na Dalorajieaga. Watu hawa wanaishi zaidi sehemu ya kaskazini ya nyanda za juu za kivolkano zinazozunguka mlima Hanang’ na Ngorongoro nchini Tanzania. Na kwa sasa wamesambaa sehemu nyingi za Tanzania mikoa ya Kati, Mashariki Pwani, Kusini na Magharibi Kusini mwa Tanzania.
Wadatooga wanafuga mbuzi, kondoo, punda, lakini ng’ombe ndiyo mnyama muhimu na anayefugwa zaidi na jamii hizi. Jamii hizi zinaiishi kwa kuhamahama; na huenda popote kutokana na mahitaji ya mifugo. Kunatakiwa kuwe na mfumo wa watumishi kuhama na makundi ya Wadatooga wanapohamia vijiji vingine.
Wadatooga wanatazamwa na jamii zingine kama ni watu wagomvi na ndiyo maana wanachukuliwa kama maadui na hivyo kupewa majina kama wamang’ati (neno la Kimasai lenye maana ya adui). Watu hawa (Wadatooga) wanajipenda sana, pia wana sifa ya kuwa wapiganaji wakali. Wameshikilia tabia zao za asili na desturi zao, ikiwa ni pamoja na mtindo wao wa mavazi na lugha zao.
Wadatooga ni wagumu kuacha mila na kubadilika, ikiwa ni pamoja na kupokea imani ya Kikristo; wakishikilia kwa nguvu zote dini yao inayoamini juu ya Mizimu – mababu waliokufa siku nyingi. Wanaamini kuwa ukifa ukiwa mzee unakuwa huna dhambi na unaenda kuishi na Mungu na unaweza kuwasaidia wanaoishi kukabiliana na changamoto zozote za maisha. Ibada za Wadatooga hufanyika sehemu ambazo wanaamini ndiko sehemu Mizimu wanaishi, mfano makabulini, kwenye baadhi ya milima.
Kwa vile Wadatooga wengi hawazungumzi Kiswahili, ambayo ni lugha ya taifa la Tanzania na wengi wao hawajui kusoma na kuandika huwa ni ngumu kuwashirikisha injili, hivyo hulazimika kutumia lugha yao. Inakadiriwa kuwa ni asilimia 2 tu ndo wanamjua Yesu na asiilimia 98 hawamjui Yesu ni nani.
Mahitaji ya Kuombea – Omba
- Kwamba Injili iweze kupenya katika maeneo ya Wadatooga, kuongezeka na kuzaa matunda kwa ajili ya Wadatooga kupata uhuru wa kweli katika Kristo kutoka kwenye dini za asili na ibada za mababu.
- Kwa ajili ya watumishi wanaohudumu katika maeneo haya ili waweze kutiwa nguvu na faraja.
- Ili kwamba Mungu aongeze watenda kazi walio tayari kwenda na kuishi miongoni mwao na kuwashirikisha injili kwa jaili ya mioyo yao.
- Kwa ajili ya waamini wapya waweze kuishika imani na waweze kuzifikia familia na jamii.
- Kwamba Mungu alainishe nafsi zao na kubadilisha mitazamo yao ili waukubali ukristo na kuacha upinzani dhidi ya Injili.