Makundi ya Watu: WWW
Watoto wa Wamishenari, wanaojulikana kama WWW, wamekuwa sehemu ya historia ya umisheni tangu zama za Umisheni wa Kisasa ulipoanza mwishoni mwa miaka ya 1700. Lakini hadi miongo ya hivi karibuni, sifa zao za kipekee na majukumu yao ya kipekee ya kimisheni yameeleweka kidogo tu na kwa sehemu kubwa hayajarekodiwa. Leo michango yao, uzoefu wao wa kipekee wa maisha na sifa zao zenye kufaa zinajulikana na kueleweka vizuri zaidi.
Uzoefu wa WWW juu ya tamaduni na watu wengine imewawezesha kuishi kipekee na kuwandaa kukabiliana na ulimwengu wa utu uzima. WWW wengi huwa viongozi makanisani, na katika huduma zingine ulimwenguni. Henry Luce alizaliwa na wazazi wamishenari nchini China mnamo 1898. Alipokuwa mtu mzima alianzisha gazeti la Time la kwanza na la aina yake na bado ni gazeti la habari linalosambazwa kila juma mpaka sasa ni moja ya gazeti linalosambazwa kwa wingi duniani. Mitazamo aliyopata kipindi cha utoto wake ilichochea maono yake katika uchapaji wa habari za kimataifa.
Neno jipya, Watoto wa kizazi kipya, liliundwa katika miaka ya 1950 na mtafiti Ruth Useem. “Mtoto wa kizazi kipya ni mtoto ambaye, sehemu kubwa ya maisha yake na makuzi na maendeleo yapo katika utamaduni tofauti na wa nyumbani kwa wazazi wake na huendeleza mahusiano na tamaduni zote, japo akiwa hana umiliki kamili katika tamaduni yoyote ile kati ya zote alizokulia. Mambo mbali mbali wanayoyaishi na kuyazoea kutoka kwenye kila tamaduni hujumuishwa kwa kadri anavyozidi kukabiliana na jamii hiyo, na hisia ya kujisikia kuwa ni mtu wa sehemu fulani husika huwa sawa na watoto wengine wanaoishi kama yeye.” Watoto wa kizazi kipya ni pamoja na WWW, watoto wa wafanyabiashara, wanadiplomasia, na wafanyakazi wengine wa kimataifa.
Watu wazima ambao ni WWW wengi hushikilia malezi yao, baraka na changamoto zao, na uzoefu wa kipekee ambao umewatengeneza. Lakini kama watoto wote wa wazazi wa Kikristo, wanaweza vile vile kuchagua kuachana na imani.
Kwa Kuangalia/Kwa UfupiÂ
- WWW hupata uzoefu na ujuzi wa kufanya kazi vizuri ndani ya tamaduni mbalimbali.
- WWW wanaweza kujisikia wametelekezwa na watu/wazazi mahali au kwenye nyumba tofauti tofauti na kukosa mahali/nyumba moja sahihi watakapopaita nyumbani.
- WWW wanatatizika kujua ni wapi wanastahili.
Mwombe Mungu:
- Kutoa mpango mzuri wa utume na viongozi wa kanisa jinsi ya kusaidia familia nzima kuingia katika wito wa Agizo Kuu.
- Kuwasaidia WWW wakati wa mabadiliko ya kuhama kutoka nchi yao hadi kwenye nchi na makazi mapya ya huduma na shule.
- Awarudishe kwake WWW ambao hawamfuati Mungu.
*Tafsiri kutoka Third Culture Kids:Â Growing up Among Worlds na David Pollock na Ruth Van Reken