Makundi ya watu Wamatumbi
Wamatumbi wapo takribani 250,000 na wanajulikana kama watu wa milimani. Milima hii hua ni ngumu kufikika, haswa msimu wa mvua na wengi wao huishi kwenye misitu. Haswa ni wakulima wa kujikimu, huvuna mpunga na kufuga kuku. Baadhi ya Wamatumbi wanaishi katika eneo linaloenda hadi kwenye bahari ya Hindi na Visiwa vya Songosongo na wao ni wavuvi. Baadhi ni wamiliki wa maduka madogo yaliyopo pembezoni mwa barabara kuu. Wanafuata mfumo dume na ndoa za mitala, ingawa talaka ni jambo la kawaida sana.
Wamatumbi ni watu huru na wanaojivunia, waaminifu, ingawa wana kipato cha chini na hawana ushawishi nchini Tanzania. Vijana wengi wanaweza kusoma na kuandika kiswahili, lakini kuna kiwango kikubwa cha kutojua kusoma na kuandika miongoni mwa wazee, ambao hutumia lugha ya kimatumbi zaidi. Wastani wa elimu huishia darasa la saba Wamatumbi ni Waislamu kwa 99%, na hufanya sherehe na kutoa dhabihu kwa mapepo/mizimu. Kuna kuenea kwa matumizi ya uchawi na hirizi vile vile. Kazi ya umisionari inaendelea miongoni mwao, kwa njia mbalimbali kwa makanisa madogo ya kidhehebu yaliyo sambaa maeneo mbalimbali. Wamatumbi si wapingaji wa Injili lakini inaweza kuwa vigumu sana kwao kumwamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi. Wale wanaomfuata Kristo wamekumbana na mateso fulani ambayo kwa ujumla hupungua baada ya muda fulani.
Kwa sasa kuna rekodi za Injili katika lugha yao, pamoja na hadithi za Biblia za mfuatano wa kimatukio iliyowekwa katika namna ya sauti, na filamu ya Yesu inapatikana pia. Injili na Matendo ya Mitume ni vitabu vilivyotafsiriwa katika lugha ya kimatumbi, na sehemu nyingine za Agano Jipya zinaendelea kutafsiriwa.
Kwa muhtasari
- Kuanzia 1904-1908, Wamatumbi waliinuka kuupinga ukoloni wa Wajerumani nchini Tanzania.
- Wana pango kubwa liitwalo Nangoma, ambalo linaheshimiwa kama makazi ya mungu muhimu anayehusishwa na kucheza na kuabudu.
- Wanaume na wanawake wanashiriki majukumu ya kilimo kwa kushirikiana.
Mahitaji ya kuombea
- Mungu awainue Wamatumbi ambao watahusika katika kuchochea vuguvugu la wanafunzi ambalo litaenea kwa wingi na zaidi.
- Wamishenari wa kigeni na wamishenari wa kitanzania, kwa ajili ya huduma yenye matunda.
- Wamatumbi watambue Yesu ni nani—Mwokozi wa karibu na wa kibinafsi, anayewapenda na mahitaji yao ya kila siku.