fbpx Skip to content

Makundi ya Watu: Gujarati

4.2 Gujarati

Wagujarati ni kundi la watu ambalo limetawanyika sana takriban katika mataifa 129 na wanajumuisha asilimia 33 ya Wahindi wote walioko ughaibuni kote duniani. Asili ya Wagujarati ni katika jimbo la Gujarat Magharibi mwa India, na lugha yao ni Gujarati. Wakiwa wamejulikana kwa karne nyingi kama wafanyabiashara na watu wanaosafiri sana baharini kwa ajili ya biashara, mara nyingi wao huwa watu wa kwanza kuhamia nchi zingine duniani. Wagujarati wanasifika kwa uwezo wao mkubwa wa kufanya biashara. Kuanzia kuwa na viduka vidogo kwenye kona za nyumba mpaka kuwa na maduka makubwa ya kuuza bidhaa za kila aina. Ustadi wa Wagujarati katika biashara unajulikana tangu zamani.

Wagujarati wametoa viongozi wakubwa duniani kama vile Mahatma Gandhi, mwanaharakati wa kihindi aliyeongoza harakati za uhuru wa India kutoka kwa Waingereza. Waziri Mkuu wa sasa, Narendra Modi pia anatoka jimbo la Gujarati.

Kwa mujibu wa sensa ya dini katika jimbo la Gujarati ya mwaka 2011, asilimia 88.5 ni Wahindu, asilimia 9.67 ni Waislamu na asilimia 0.52 ni Wakristo. Asilimia inayobakia ambayo ni ndogo chini ya 2, inachangiwa na dini za Sikhs, Budha na Wajain kwa pamoja.

Dini ya Kihindu, ambayo ndiyo dini kubwa nchini India, ni dini kongwe ambayo imekuwepo tangu miaka 3000 kabla ya kuzaliwa Kristo, na leo ni dini ya tatu kwa ukubwa duniani baada ya dini za Ukristo na Uislamu. Dini ya Kihindu ni mchanganyiko wa imani na falsafa, na inaamini uwepo wa miungu mingi inayofikia milioni 33. Baadhi ya wanazuoni wake, huiita dini hii ‘njia ya milele’.

Kwa mtazamo

  • Wahindi wa Gujarati ni kundi la watu lililotawanyika sana, wakipatikana angalau katika nchi 129 kati ya nchi 190 zilizopo duniani.
  • Wagujarati wamejaliwa kuwa na uwezo mkubwa katika biashara.
  • Asilimia 88.5 ya Wagujarati ni Wahindu, ilhani wakristo ni asilimia dogo, kama vile 0.52.
  • Kimsingi wafanyabiashara, huwa wamejiweka wazi sana katika kujichanganya na watu wengine, baadhi yao wakiwa Wakristo.

Mwombe Mungu:

  • Achochee upendo wa majirani wakristo kwa jamii ya Gujarati.
  • Ageuze macho ya Wagujarati kutoka kwenye njia za upotovu wa milele na badala yake awafunulie njia, kweli na uzima – Yesu.
  • Afungue macho watu waone Ukuu wa Kristo. Kama wahindu, waweze bila ubishi kumpokea Kristo, siyo kama mmoja wa miungu yao mingi. Pia, wasije wakatafsiri vibaya mwito wa kuzaliwa upya kama aina ya mtu kutokea tena kuwa kiumbe tofauti baada ya kufariki dunia bali wampokee kama Mwokozi pekee wa roho na waelewe kuzaliwa mara ya pili kwa ajili ya uzima wa milele.
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us