Mafunzo ya Umisheni
East Africa School of Mission (EASM) ni chuo kilicho chini ya bodi ya wachungaji ya mafunzo ya utume. Inayotoa mafunzo ya umisheni kuanzia ngazi ya cheti, diploma na shahada. Chuo hiki kilianza 2015 kama shule ya utume ya kwanza nchini Tanzania, mkoa wa Dar es salaam. Lengo la kutoa mafunzo ya umisheni yaani utume wa kuwafikia wasiofikiwa.
Chuo kilianza kutoa wahitimu wa umisheni wa kuwafikia wasiofikiwa. Wachungaji, Wainilistini na Maaskofu waliojiunga kwa mwaka 2015 kwa ngazi zote zilizotajwa hapo juu ambao walipata umaarufu mkubwa kama wachungaji wenye elimu na uwezo mkubwa katika ufahamu wa utume wa kuwafikia wasiofikiwa kwa Afrika.
Mwaka 2016, chuo kilihamia katika majengo ya chuo cha kanisa la Kibatisti kinondoni B. Hii ilisababishwa na umbali uliokuwepo kwa wanafunzi wa kutwa kufika vikindu na kurudi mjini, na miundo mbinu kutokuwa rafiki sana kwa wakati huo. Mwaka 2017, chuo kilihamia Pugu Kajiungeni katika majengo ya kanisa la Shinglight Church, ambapo ndio kipo mapaka sasa. Hii ni kutokana na wanafunzi kuongezeka. Masomo ya vitendo ya ujasilia mali yalaianzishwa (kushona mahema) mafunzo haya hutolewa kwa mwaka mmoja kwa ngazi zote.
Chuo kimeendelea kukua na kutanuka na kupata umaarufu mkubwa ndani na nje ya ya mipaka ya Tanzania. Chuo kiliendelea kutoa mafunzo bora sana kwa wamishenari, wainjilisti na wachungaji, yanayohusu utume/umisheni wa kuwafikia wasiofikiwa. Chuo kimekuwa na wanafunzi kutoka Tanzania, Burundi, Congo ya DRC, Sudan kusini n.k. Chuo kina mabweni na madarasa pamoja na walimu wa uhakika kutoka ndani na nje ya Tanzania na Afrika.
Karibu ujiunge nasi, mawasiliano yetu ni;
- Bishop Eliasaph Mattayo: +255655501202 eliasaph.mattayo@gmail.com (Mwnyekiti)
- Mch. Samwel Kengela: +255754 615853 kengelasaam@gmail.com (Mkuu wa chuo)