fbpx Skip to content

Kozi ya Kairos

Kozi imeandaliwa ili kuelimisha na kutoa changamoto kwa wakristo na kulitia moyo kanisa kuitikia moyo wa Mungu kwa ajili ya umisheni kwa mataifa. Kairos inaelekeza na kuongoza huduma yenye mwamko na yenye maana katika kuvuka mipaka ya tamaduni na kuwa na nia ya kuwafikia wale ambao hawajafikiwa na habari njema za Yesu katika jamii zetu ili kumfanyia Mungu ibada.

Kairos inalenga maeneo manne ya umisheni ambayo ni: Msingi wa Kibiblia, Mtazamo wa Kihistoria; Mwelekeo wa Kimkakati; na hali ya Kiutamaduni. Inatumia zana za kuwawezesha kutimiza wajibu wao kikamilifu katika kufundisha, majadiliano, na mihadhara mifupi. Mafunzo ya Kairos yanaweza kukusaidia wewe na kanisa lako kufahamu kusudi la milele la Mungu juu ya umisheni toka kwenye kitabu cha Mwanzo mpaka Ufunuo wa Yohana. Wawezeshaji waliopata mafunzo na wenye hadhi ya kimataifa hufundisha kozi hii. Washiriki watasajiliwa na kupewa mbinu kwa ajili ya waliopotea.

Kwa Tanzania, kozi ya Kairos hutolewa kwa wiki moja kwa wachungaji, wainjilisti na wakristo waliojitoa wa madhehebu yote. Mafunzo haya hutolewa katika mikoa yote kwa lugha za Kiswahili and Kingereza. Kwa maelezo zaidi wasiliana na waratibu, Silas Brandl kwa barua pepe silas_brandl@gmx.de na Julius Rukya kwa simu namba +255754826533.

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us