Skip to content

“Mazingira ya maeneo ya Uislamu yanahitaji uvumilivu” – nyakati za wamishenari

The Fellowship of Christian Unions (FOCUS) nchini Kenya ni shirika kubwa ambalo huwa linawafunza wanafunzi na viongozi wa Kikristo kutoka miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu. Uzoefu wao wa Muda Mfupi katika mpango wa huduma (STEM) programme ambao huwatuma vijana kusaidia katika huduma kwenye jamii na makanisa. Mwaka huu, tulipokea ripoti kutoka kwa wasichana kadhaa ambao walienda kufundisha katika shule iliyoko kati ya watu ambao hawajafikiwa na wakimbizi. Kila mmoja wao aliripoti hatua nzuri za kufaulu kitaaluma miongoni mwa wanafunzi wao, lakini pia kupendezwa na mambo ya kiroho kwa watoto pia kuunda uhusiano katika jamii. Sally, ambaye alihudumu katika kambi ya wakimbizi, alikuwa na haya aliyobainisha wakati akihudumu:

1. Kuhudumu katika mazingira yenye Waislamu wengi kunahitaji uwe na uvumilivu, uwe mwelewa, na uwe mwenye utambuzi ili kuihubiri injili.
2. Kujenga uhusiano thabiti ndani ya jamii kunawezesha kukuza uaminifu na kufungua fursa za majadiliano ya imani na yenye maana.
3. Kuwa na muda binafsi wa Ibada thabiti ni muhimu sana kwa kushibisha roho na kuwa na huduma yenye matokeo.
4. Kuyazoea mazingira mapya ya huduma kunaweza kuwa na changamoto, lakini pia kunaweza saidia kujiimarisha zaidi na kutoa fursa za kukua.

Masomo kama hayo ni yenye thamani sana kwa Wakristo wachanga, wanapoendelea kupata uzoefu na namna ya kufikiria huduma yao wakati ujao! Uzoefu wa muda mfupi mara nyingi huwa ni wakati muhimu kwa vijana, na huwaongoza katika kutafakari kwa uzito wito wa Mungu katika maisha yao. Hata kama hawatakuja kuwa Wamishenari wa wakati wote katika siku za mbeleni, kuna uwezekano mkubwa wa wao kuwaombea watu waliopotea na kuja kuwa wanawasaidia kifedha wamishenari.

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us