fbpx Skip to content

Biblia ya kiarabu cha Kichadi yachapishwa

Biblia yote ya Kiarabu cha Kichadi imetafsiriwa na kuchapishwa kwa mara ya kwanza. Kupatikana kwa tafsiri hii ya Biblia kulisherehekewa hapo mwezi Aprili 2021 pamoja na matukio mawili ya kuwekwa wakfu katika mji mkuu wa Chad, N’djamena. Zaidi ya Biblia 100 zilifika sehemu za Mashariki mwa nchi ya Chad mwezi Mei 2021, mahali ambapo timu ya SIM ipo. Shehena ya pili ya Biblia iliwasili mwezi Oktoba 2021. Mfanyakazi wa SIM, alinukuliwa akisema, “Sisi na wafanyakazi wenzetu ambao ni mmishenari hapa Chad tumefurahi sana kuwa na Biblia katika lugha ambayo watu wengi katika eneo hili la Dar Sila wanaielewa.’’ Kiarabu cha Kichadi ni aina ya lugha zenye mchanganyiko na kifaransa na ndiyo lugha ya nchi na sehemu ya kusini mwa Chad ambayo wakazi wake wengi ni Waislamu. Tafsiri ya Biblia hii imechukua zaidi ya miaka 20 kwa ushirikiano kati ya makanisa ya Chad, mashirika ya kimisheni ya Wycliffe na WE International. Mradi huu pia uliungwa mkono na jamii kubwa inayozungumza Kiarabu. Wachad pia wataweza kupata Biblia hii ya Kiarabu kupitia hata kwenye simu zao za mkononi zenye Tafadhali ombea usambazaji wa Biblia hizi katika nchi yote ya Chad, na hasa kwenye maeneo ambayo yana Waislamu wengi ambao kwa muda mrefu hapakuonekana uhitaji wa Biblia. Kwa taarifa zaidi kuhusu tafadhali tembelea: https://bit.ly/3Iy3HY1.

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us