fbpx Skip to content

Kuwashuhudia Waislamu kwa hekima

Jared Oginga

1. Hofu na Ujinga: Tafuta kuujua Uislamu kama mfumo, na Waislamu kama watu waliopendwa na Mungu, lakini wamenaswa kwenye mtego wa mfumo wa dini. Ujinga na hofu kutoka kwa Wakristo ndivyo vinavyozuia kazi ya kuwashuhudia Waislamu. Mwislamu atafahamu Injili kwa kiwango kile ambacho wewe unafahamu imani yako na yeye kama mtu.

2. Jenga mahusiano ya kweli na upendo wa kweli na Waislamu (Warumi 2:9): Uinjilisti kwa Waislamu kimsingi umejikita kwenye kujenga mahusiano ya kweli na urafiki. Jitahidi kufahamu kazi yake, familia yake, marafiki n.k., na fanya hivyo kwa undani kabisa. Jaribu kujua hofu zake, furaha, na mapambano yake ya maisha ya kila siku na matumaini yake. Uhusiano wa namna hii unatakiwa utokane na upendo, ili ajisikie upendo wa Kristo ndani yake.

3. Jenga kuaminiana: Wakristo siyo binadamu bora kupita binadamui wote; tuna upungufu wetu kama binadamu. Mweleze rafiki yako Mwislamu ukweli na jinsi neema ya Mungu inavyokusaidia wewe kuishi maisha ya kikristo.

4. Inachukua Muda: Kila kitu unachomwambia mwislamu analinganisha na alichofundishwa kwenye dini yake. Ujumbe wa Injili siyo tu unatakiwa kuonekana ni wa maana kwa Mwislamu bali unatakiwa umfanye kuona hitaji la kuupokea tofauti na alichonacho.

5. Usipuuze maswali yake: Kweli zote za kibiblia lazima zielezwe vizuri na kueleweka; kusiwe na ukweli wenye ubabaishaji. Kuacha imani yake na kuwa mkristo ni uamuzi mgumu ambao muiislam anaweza kuufanya katika maisha yake, na katika hili atataka kuwa na uhakika wa uamuzi wake.

6. Nenda naye pole pole hatua kwa hatua: Hisia zake na hofu siyo tu kwamba ni za kidini; nyingine ni za kibinafsi. Anahitaji uhakika, mwongozo na pia usaidizi.

7. Makabiliano au makaribisho? Injili ni kinyume na kile ambacho Uislamu unamuahidi mwanadamu, na kwa hiyo kutakuwa na maeneo ya kutofautiana. Usikwepe maswali magumu. Jaribu kujibu maswali yote kibiblia kwa kadiri unavyoweza. Kama huna jibu la kibiblia, usivumbue la kwako. Uwe mkweli. Hakuna mkristo ambaye ndiye kipimo cha uhakika cha Ukristo.

8. Jaribu kujiongeza: Mtu anaweza kutumia muda mwingi na Mwislamu na wala isieleweke ni mada gani imezungumzwa na kumalizwa. Jaribu kuanzisha mada, na kamwe usijibu tu maswali yasiyohusiana na mada husika katika mazungumzo yenu.

9. Mshirikishe kwa uchache: Kama vile msemo usemao, “mwalimu mzuri hafundishi kila kitu anachojua; badala yake anajua anachofundisha.’’ Mshirikishe kile unachojua kwa sehemu na kwa wakati maalum; Mwislamu anahitaji muda kufikiri juu ya yote unayojadiliana naye.

10. Fanya maombi kuwa ndiyo silaha yako kuu: Hii ni vita kati ya uzima na kifo, nuru na giza, Mungu na Shetani. Siyo hoja zetu za mabishano, bali ni Roho Mtakatifu ambaye atawashawishi Waislamu kuona haja ya kumkubali Yesu kuwa Mwokozi wa maisha yao.

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us