fbpx Skip to content

Ninawi yamsubiri kila Mkristo

Jared Oginga

Umeshawahi kufikiria kwa nini Yona alipata misukosuko yote ya kwenda kuwaonya wakazi wa Ninawi juu ya hukumu, katika mji ambao ulikuwa na wakazi 120,000 tu? Leo inakadiriwa kuwa kuna Waislamu wapata o bilioni 1.8 ulimwenguni kote, ambapo kati yao milioni 446 wanaishi katika bara la Afrika pekee. Mungu anawapenda hawa Waislamu pia, lakini bado hawajamjua na kuonja pendo lake. Mkristo wa kawaida ana ufahamu mdogo sana juu ya Uislamu na Mwislamu. Watu wengi wanawaogopa Waislamu kutokana na hali tete ya asili katika uhusiano kati ya Wakristo na Waislamu. Hata hivyo, wengi wa Waislamu hufurahia mazungumzo au mijadala ya kidini pamoja na Wakristo. Pengine, kama ilivyokuwa kwa Waninawi, Waislamu wako huru kuzungumza kuhusu masuala ya kidini kuliko tunavyofikria.

Kwa nini Tuwafikie Waislamu?

Kwa ujumla, watu wanafikiri kuwa ni vigumu kwa Mwislamu kuja kwa Kristo. Lakini hii si ndivyo ilikuwa hata kwetu kabla ya kuokoka? Ugumu huu kwa kiasi fulani unatokana na asili ya dini yenyewe ya Kiislamu, ambayo hufanya kazi kwa mfumo kama vile chanjo. Uislamu ni dini ambayo humpa Mwislamu nusu ukweli kuhusu Mungu, ili anapokutana na ukweli halisi basi akili zake huusukumia mbali au kuujua ukweli. Inahitajika juhudi kuweza kuvunja kizuizi hiki.

Habari ya Yona hunisisimua. Yona alipotumwa kwenda Ninawi, si tu kwamba hakuwa tayari bali alikimbilia kwenda upande mwingine. Leo baadhi ya makanisa na waumini wanakaidi uharaka huu wa kazi ya kuwafikia Waislamu wakati wengine wakiu kimbia kabisa wajibu huu.

Kama ambavyo BWANA alituma samaki mkubwa kwenda kummeza Yona, tunajua anaweza kuziba njia za watumishi wake kuukimbia wito.

Leo kundi kubwa la watu ambao bado hawajafikiwa ni la wale ambao hujitambulisha kama Waislamu, ambao kama Kristo angerudi leo hatima yao ingekuwa ni kuishi mbali na Kristo.

Je, kanisa linajali kuhusu kuwafikia Waislamu kama inavyotakiwa?

Nilijiunga na shirika la Life Challenge Afrika nikitokea chuoni, kama mratibu wa mahusiano watu. Siku moja nilizuru moja ya makanisa makubwa katika Jiji la Nairobi kukuza na kuhamasisha kijitabu cha siku 30 za maombi kwa Waislamu.

Watu wanafikiri kuwa ni vigumu kwa Mwislamu kuja Kristo. Lakini hii si ndivyo ilikuwa hata kwetu kabla ya kuokoka?

Mchungaji Mwandamizi alikuwa akikagua ujenzi hapo kanisani kwake. Nilimweleza kwa nini kanisa linahitajika kujihusisha na Waislamu na hata kuwekeza pesa ili kupata vitabu vya maombi- ili kuwaombea Waislamu wakati wa mwezi wa Ramadhani.

Mchungaji alinisikiliza kwa makini. Baada ya kumaliza, alinionyesha kwenye kona ya eneo la ujenzi na kusema kwa upole, ‘‘kijana [nilikuwa kijana mdogo wakati huo] unavi ona vile vyoo? Tunahitaji kumaliza hivyo kwanza. Rasilimali zetu zote za pesa tumezielekeza kwenye mradi huo.’’

Nilihuzunika, lakini niliweka kusudio kutembelea tena kanisa hilo. Leo, kanisa hilo siyo tu linaomba kama mwanzoni nilivyoomba bali ni moja ya makusanyiko ambayo yanaelekeza rasilimali watu na pesa kuwafikia Waislamu katika Kenya na nje ya Kenya.

Kwa nini kanisa liwajali Waislamu? Swali hili lina majibu mawili. Kwanza, kusudi la msingi kwa kanisa ni kumfanya Kristo kujulikana kwa wale ambao bado hawajasikia Injili (Matendo 1: 8). Kwa hiyo, kanisa lipo kwa ajili ya wasioamini. Kama kanisa haliwafikii wale walioko nje ya kuta zake basi hapo tunamwangusha Bwana Yesu.

Pili, Waislamu ni sehemu kubwa ya watu ambao hawajafikiwa kabisa. Ili kanisa la Afrika lionekane kweli linashughulika na umisheni, ni lazima liwafikie Waislamu.

Kuwafikia Waislamu kunahitaji mafunzo ya msingi katika kuujua Uislamu, kujua kuitetea imani ya kiKristo na kuwa na njia za matendo.

Kanisa Lianzie Wapi?

Kwa kuanzia, kanisa linapaswa kumuhamasisha kila mkristo; huduma ya injili kwa Waislamu haijahifadhiwa kwa ajili ya watu wachache tu. Mwitikio wa kwanza ni kufanya maombi kwa bidii. Pili, kanisa lazima litenge rasilimali fedha ili wale wenye shauku ya kuwafikia Waislamu waweze kupata mafunzo na kuandaliwa kwa kazi hiyo.

Kwa vile tunamtumikia Mungu mwenye upendo, anayejali na kutamani watu wote wapate maarifa ya kumjua Kristo anayeokoa, sisi tulioitwa kwa jina lake hatuna uchaguzi bali kuwapenda Waislamu kikweli kweli, kuwaombea kila mara, na kuteka kila fursa kuwashirikisha habari za Kristo kwa njia ya ufasaha.

Jared Oginga ni makamu Mkurugenzi wa Shirika la Life Change Afrika ambapo amelitumikia kwa miaka 22 sasa. Mtembelea kupitia: https://life-challenge.org/ Barua pepe: jared.oginga@sim.org.

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us