fbpx Skip to content

Kwa nini: tuwafikie Waislamu?

Ray Mensah

Hivi majuzi niliombwa kufundisha kozi juu ya ‘Ukristo na Dini zingine za Ulimwengu’ katika Taasisi moja ya kitheolojia. Nilipokuwa naandaa somo la kufundisha, nilibahatika kusoma makala iliyoandikwa na kiongozi wa huduma ambaye anawafikia Waislamu. Alikadiria kuwa asilimia 99 ya Wakristo hawajui namna ya kuwaeleza Injili watu wa imani zingine. Takwimu hizo za kushangaza zilinifanya nifikiri. Kitabu chenye taarifa za kikristo za Ulimwengu (Encyclopedia) kinaeleza kuwa asilimia 81 ya watu ambao si wakristo hawamjui mtu anayeitwa mfuasi wa Kristo. Nilikubali kuwa Kiongozi huyu wa Misheni anaweza kuwa hayuko mbali na ukweli.

Baadhi ya makanisa, mashirika ya umisheni, vituo vya mafunzo na wamishenari wanajifunza namna maalumu ya kuwafikia Waislamu, na kwa kweli wanafanya kazi nzuri. Tunawapongeza sana wao pamoja na wainjilisti na wamishenari hawa wenye ujasiri.

Pia kuna kozi nzuri sana pamoja na vitabu vingi vizuri (angalia vitabu vingi vimetajwa kwenye ukurasa wa 8 & 9). Rasilimali hizi zinapaswa kupatikana kwa urahisi kwa mwili wa Kristo katika kuwawezesha mamilioni ya wafuasi wa Kristo kuwafikia Waislamu kikamilifu. Hili ni suala la haraka na ni wito unaotutaka tuchukue hatua.

Sababu kuu mbili kati ya nyingi za kwa nini Wakristo hawawafikii Waislamu na Injili ni hofu na upungufu wa maarifa juu ya namna bora ya kuwashuhudia habari za Injili. Mkristo wa kawaida anaweza kumshuhudia mkristo dhaifu habari za Kristo lakini atamruka mwislamu. Asilimia kubwa ya Wakristo wanafikiri wao na Waislamu wanaamini Mungu huyo huyo mmoja na kwa hiyo hawaoni hitaji la kuwahubiria Waislamu. Hali hii inatakiwa kusahihishwa na wachungaji wetu katika makanisa yetu.

Bwana wetu Yesu Kristo alisema wazi katika Mathayo 9:38 kuwa ‘mavuno ni mengi lakini wavunaji ni wachache’. Mavuno haya ni pamoja na Waislamu. Mavuno ya Waislamu ni mengi lakini wavunaji wa kuwafikia ni wachache.

Kwa miaka mingi, kinyume na mitazamo ya watu, nimekuja kujua kuwa, Waislamu wengi wako wazi kwa Injili na wengi wao wako tayari kuu jua ukweli.

Tunahitajika kuomba kwa bidii ili BWANA wa mavuno ainue wamishenari kuwafikia Waislamu na wokovu kwa Waislamu ufike kote Afrika na ulimwenguni. Baadhi ya Waislamu wanakutana na Bwana Yesu kupitia ndoto na maono na wanaokoka kwa sababu mtu fulani aliwaeleza habari za Injili na aliwaombea kwa nguvu zake zote.

Kuna sababu kadhaa ambazo zinatufanya tuwafikie Waislamu; nitasema mbili tu. Ya kwanza, Kristo alilipa kanisa agizo kuu. Lazima tuwafanye mataifa kuwa wanafunzi wa Kristo (Mathayo 28:18-20), na ni lazima twende ulimwenguni kote kuhubiri Injili kwa kila mtu (Marko 16:5). Kwa hakika, kila mtu ikiwa ni pamoja na Waislamu.

Pili, Waislamu ni kundi kubwa la watu ambao bado hawajafikiwa katika ulimwengu. Kwa mujibu Kwa mujibu Joshua Project, kuna Waislamu wapatao bilioni 1.8 duniani kote na kuna makundi ya Waislamu yapatayo 3,467 ambayo bado hayajafikiwa na injili.

Ray Mensa Mensah anatumika kama Mkurugenzi wa shirika linaloitwa ‘One Way Africa’ na ni Rais wa GEMA. Pia ni Mhariri wa Gazeti la Sauti ya Umisheni anayesimamia Shule ya Umisheni ya Jiwe Lililo hai. Unaweza kuwasiliana naye kwa: ray@owm.org

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us