fbpx Skip to content

Walioitwa: Septi Bukula – Kusudi la Biashara ni nini?

Nilipoulizwa swali hili yapata miaka 14 iliyopita, nilifikiri nilijua Jibu lake. Wakati huo nilikuwa nahudhuria kongamano huko Jakarta nchini Indonesia, pamoja na waumini kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni. Baada ya juma moja la majadiliano, hatimaye tulikuja kufikia hitimisho moja: kusudi la biashara ni kumtukuza Mungu.

Huo ulikuwa ni mwanzo wa safari. Swali lililofuata lilikuwa: Je, biashara inayomtukuza Mungu inatofautiana vipi na biashara ambayo haitafuti kumtukuza Mungu? Imenichukua miaka kadhaa kufikia mahali pa kupata baadhi tu ya majibu.

Baada ya majibu hayo, nilipata mwanzo wenye nguvu katika biashara na huduma, miaka mingi kabla ya kupata maneno haya, Biashara Kimisheni (Missional Business, MB) kuundwa. Baba yangu alikuwa mtu wa ajabu – mtu pekee aliyekuwa m c h u n g a j i muda wote, m f a n y a b i a s h a r a muda wote na mkulima muda wote. Hivyo ndivyo alivyolea watoto wake wanane. Yeye na mama yangu waliongoza makanisa 20 ya mtaa katika mtindo wa zamu. Kwa sababu kwa hakika tunaweza kusema walikuwa hawalipwi, ilibidi watafute namna ya kuhakikisha familia inapata chakula. Baba yangu aliniambia, ‘Mwanangu, situmii pesa ya kanisa kuendesha familia yangu; bali ninatumia pesa ya familia yangu kuendesha kanisa’.

Shughuli za baba yangu zilizidi hata chakula cha kujikimu; alikuza mahindi, na alikuwa na mifugo, lakini kwa kiwango kidogo tu cha kibiashara. Kama watoto, kila mmoja wetu alipewa sehemu kubwa ya eneo na tuliwajibika kulima mazao ya biashara – kama vile kabichi, nyanya – huku tukifanya kila liwezekanalo ili kupata mavuno. Tuliuza mazao yetu kwenye masoko madogo mahali ambapo baba alikuwa anapajua. Tulimlipa mwenye nyumba kupata eneo la kuhifadhia mazao yetu. Baba yangu alihakikisha tunawajibika kwake kwa namna tulivyokuwa tunatumia pesa zetu.

Wakati wa mavuno, baba yangu aliweka sharti moja. Tulipaswa kufunga mfuko uliojaa mboga, kisha kununua sukari, majani ya chai, mafuta ya kupikia, na kupeleka mzingo wote huu kwa familia maskini. Hii ilikuwa ni kabla ya kujua utoaji zaka, wazazi wangu walinifundisha kuwa kama una vingi, unapaswa kuwapa wengine.

Injili ya Mafanikio imefanya uharibifu mkubwa kwa kuwafundisha watu kuwa Mungu yupo kwa ajili ya kuwabariki wao binafsi. Hii ni kinyume na mafundisho sahihi ya Biblia. Tunabarikiwa ili tueneze baraka kwa wengine! Kukabidhiwa na Mungu kwa baraka ni kukabidhiwa kwa kupewa wajibu wa kushirikisha baraka hiyo na wengine – siyo tu na familia yako au jamaa zako wa karibu, bali na jamii kubwa iliyobakia katika ufalme wa Mungu. Nawahimiza wafanyabiashara kujiuliza wao wenywe, “Je, naiona biashara yangu kama yangu tu, au kama biashara ya Mungu ambaye amenikabidhi kuiendesha?”

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara haijaunganishwa na kazi za umisheni. Biashara Kimisheni (MB) inabakia kuwa ni mazungumzo miongoni mwa jamii ndogo tu ya wafanyabiashara. Wamishonari na wafanyabiashara wanaishi katika sehemu mbili tofauti za dunia. Niliamua kuratibu tukio ambalo lilileta watu pamoja kutoka ulimwengu wa aina hizi mbili. Hivyo, huduma ya Injili ya Wekeza Afrika (Mission Invest Africa- MIA) ilifanyika mwaka 2018 huko Johannesburg, Afrika Kusini.

Kimakosa, wengi wanaamini kwamba biashara na Ufalme wa Mungu havichanganyiki, na hii inazuia fursa kubwa katika kuendeleza ufalme wa Mungu. Hali hii ya kutoelewana imesababishwa na makanisa ambayo yameweka utengano kati ya eneo takatifu na lile la kidunia. Watu wameaminishwa kuwa kufanya biashara siyo wito mkuu wa Mungu. Lakini vuguvugu la Biashara Kimisheni (MB) linaloshika mizizi leo linasahihisha upotofu huo.

Wengi wamefundishwa kwamba tunaweza kutenganisha shughuli zetu kwenye idara mbili tofauti, yaani ‘idara yangu’ na ‘idara ya Mungu’. Biashara inaangukia chini ya ‘idara yangu’. Tumeshindwa kuwafanya wafanyabiashara kuwa wanafunzi wenye mtazamo wa biashara kimisheni. Wamekua, hata katika makanisa yetu, wakifikiri kuwa biashara ni kwa ajili ya kupata utajiri tu. Kimaandiko, hii siyo kweli.

Kilicho kweli ni kwamba dunia na kila kilichopo ndani yake ni mali ya Bwana (Zaburi 24: 1). Hivyo, biashara ni mali ya Bwana. Kama unaendesha biashara, basi ni Mungu aliyekuweka hapo. Unashikilia sehemu hiyo ya ufalme kwa niaba yake.

Kwa hiyo, nini sasa unafikiria kuwa ndilo kusudi la biashara? Kama unakubali kuwa biashara ni kwa ajili ya kumletea Mungu utukufu, hiyo inamaanisha nini kwa biashara yako leo?

Septi Bukula ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Hodhi ya Osiba (Osiba Holdings), ambayo hujishughulisha na maendeleo ya utafiti, ushauri na biashara utalii, ambayo ipo Johannesburg, Afrika Kusini. Jiunge na Wekeza Umisheni Afrika.  Facebook  na  https://www.facebook.com/www.missioninvestafrica.osiba.co.za/

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us