fbpx Skip to content

‘Njoo Huku Utusaidie’

Ni nani bora zaidi kuwafikia Waislamu wa Afrika isipokuwa Wakristo wa maeneo mengine ya Afrika? Hayo ndiyo yaliyokuwa mawazo ya mwaka wa 2011 wakati wa Mkutano wa Vuguvugu la Mkakati wa Mataifa ya Afrika (MANI), ambalo lilizalisha kwa mkakati wa Nenda Kaskazini*.

Asilimia 63 ya Waafrika wanaoishi kusini mwa Sahara wanajitambulisha kama Wakristo, ilhali zaidi ya asilimia 90 ya Afrika Kaskazini ni Waislamu. Mamilioni ya Wakristo kwa wastani wanaishi kwa amani Kusini, lakini wachache walioko Kaskazini wako kwenye adha na mateso. Katika Matendo ya Mitume 16:9, mtu mmoja kutoka Makedonia alionekana kwa ndoto akimsihi Mtume Paulo kwa kusema, ‘Njoo huku utusaidie’!. Vivyo hivyo, yanaashiria mateso wanayopata Wakristo wa Afrika ya Kaskazini.

Mkakati wa Nenda Kaskazini ulitokana na wazo kwamba Waafrika wana sifa ya pekee kuwahudumia ndugu zao katika sehemu zingine za bara la Afrika. Wakristo wanaoishi katika Afrika ya Kaskazini walilipokea wazo hili na mwaka 2015, Mshikamano wa kutoka Kusini kuelekea Afrika Kaskazini Nenda Kaskazini ulizinduliwa. Huku viongozi wa makanisa kutoka Kaskazini wakianzisha mahusiano na mashirika na makanisa ya Kusini, ili kuweza kuwaleta pamoja wafanyakazi walioko katika nchi za sehemu ya Kusini mwa Sahara.

Mchungaji Yohana, kutoka Afrika ya Kusini, yuko katika timu ya uongozi wa Nenda Kaskazini na Kanisa la Afrika ya Kaskazini. Anasema, ‘Tunaishi kana kwamba baadhi ya milango imefungwa kwa Mungu. Tumeunda misemo kama vile, “nchi zilizofungwa’’, badala ya kutaja tu makundi ya watu ambayo bado yanakosa Injili. Kwa mwitikio, Nenda Kaskazini ina maono ya kutupa changamoto na kubadilisha namna tunavyofikiri na kutendea kazi yetu… Kwa sababu hii, tunasema, “Njoo uone!’’

4.2 Come Over2

Malengo ya Nenda Kaskazini ni ya aina mbili: Kwanza, ni kuwatia moyo Wakristo kutoka Kusini kwenda kuishi Kaskazini, wakiendesha biashara zenye mlengo wa uenezaji wa injili ili waweze kujitegemeza wenyewe. Hawa wajasiriamali wanatumwa na makanisa yao ya nyumbani kwenda kwenye makanisa yaliyowapokea. Makanisa yale huwasaidia kupata makazi katika jamii na kuwapa mkono wa ushirika na kuwatia moyo ili waweze kuishi katika jamii za huko Kaskazini. Kanisa linalowatuma huwapa msaada wa kifedha kwa kadiri inavyohitajika, pamoja na kuwategemeza kwa maombi na kuendelea kuwatia moyo kutokana na kuwa wako mbali nao.

Lengo la pili ya mwelekeo wa Nenda Kaskazini, ni kuwatia moyo wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka Kusini kwenda kusoma katika Vyuo Vikuu vilivyoko Kaskazini, mahali ambapo wanaweza kuwafikia watu walio karibu na vyuo hivyo kwa njia ya ushuhuda wa imani yao. Kwa pamoja, wafanyabiashara na wanafunzi wanategemewa kuishi mtindo wa maisha ya kikristo, huku wakiendelea kuwa sehemu mpya ya jamii ya Kaskazini.

Mkakati wa Nenda Kaskazini una wanachama kutoka Mashariki, Magharibi, Kati, na Kusini mwa Afrika, ikiwa ni pamoja na ndugu kutoka mabara mengine katika kuunga mkono mkakati huu. Hadi leo, wengi wa wale ambao tayari wameshatumwa kwenda Kaskazini, wanatoka nchi za Afrika Magharibi kutokana na faida waliyonayo ya kuzungumza lugha ya Kifaransa, ambayo ndiyo lugha inayohitajika huko Afrika Kaskazini. Kila Mkristo mfanyakazi huungana na kanisa lililopo huko, na hasa wajibu wao siyo kuanzisha makanisa mapya, bali kumshuhudia Kristo katika jamii zao mpya na kushika mkono Kanisa la huko Afrika ya Kaskazini.

Mike ni Mkurugenzi Mtendaji wa Ushirika mwingine kule Kusini na ambaye ndiye sauti inayoongoza katika mkakati huo wa Nenda Kaskazini, anasema,

 Kwa nini Mungu aweke Wakristo zaidi ya milioni 40 kutoka makanisa ya Kiinjili katika sehemu ya kusini mwa Sahara ya Afrika, akiwa amewawezesha kuwa na uongozi wenye uwezo na rasilimali zinazoweza kufikia Afrika yote na ulimwengu na Injili? Kwa nini Mungu aweke rasilimali hiyo kubwa mno ya watu karibu kabisa na watu wenye mahitaji, ambao ni Waislamu waliofikiwa kidogo huko maeneo hayo? Mungu ana ajenda kwa ajili ya kanisa la sehemu ya kusini mwa Sahara na hata huko ughaibuni ambapo wapo Waafrika wanaoweza kutimiza wajibu muhimu katika hatua ya mwisho ya kupeleka Injili Kaskazini na kwa mataifa mengine ambayo bado hayajafikiwa na Injili’.

4.2 Come over3

Mkakati wa Nenda Kaskazini pia unasaidia Wakristo Waafrika ambao wamepoteza kazi kwa sababu ya imani yao katika Kristo Yesu. Mateso kwa Wakristo yanaendelea katika maeneo mengi; na usalama kwa Wakristo bado ni jambo kubwa la kuzingatia. Na kwa kweli bado ni hatari na kamwe si vema kuchapisha au kuwatambulisha wafanyakazi au Wakristo wenyeji kwa ajili ya usalama wao. Ingawa hatutakiwi kuishi na roho ya woga (2 Tim. 1:7), hatutaki kutoa fursa kwa wale ambao ni maadui wa Injili kutotuelewa.

Licha na masuala haya ya usalama, Nenda Kaskazini imetengeneza utaratibu unaoitwa Uzoefu wa “Njoo uone”. Hii ni safari fupi ambayo hufanyika kila mwaka kule Kaskazini na ni kwa ajili ya wachungaji na viongozi kutoka Kusini mwa Sahara, na mtu yeyote anayependa kazi ya injili kuja na kujionea kinachoendelea na nini kinahitajika huko Kaskazini. Safari za kutembelea maeneo ya kihistoria hutufanya kuona na kutambua kuwa Afrika Kaskazini ina utajiri mkubwa wa historia ya Ukristo, kitu ambacho kimefunikwa na kusahaulika kwa sehemu kubwa.

Richard, ambaye ni raia wa Afrika Kusini aliyeko kwenye timu ya Nenda Kaskazini alihojiwa kwa ajili ya makala haya, naye analisihi Kanisa la Afrika ‘kutafuta uhalisia juu ya maisha ya kikristo- na siyo tu kufikiria jamii yako mwenyewe. Fikiria juu ya wale wanaoishi maeneo ambayo kuwa mkristo ni sawa na kukabiliana na matatizo makubwa yasiyoelezeka. Unapaswa kujua nini kinahitajika kusaidia sehemu zingine za ulimwengu’.

Wakristo walioko Kusini mwa Sahara kwa kweli wanasikia wito kutoka Kaskazini wa, ‘Njoo huku utusaidie’! Na wanauitikia wito huo.

Kuna Wakristo huko Kaskazini, lakini ni wachache. Wanahitaji ndugu kuja na kusimama pamoja nao. Kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu hatua inayofuata juu ya Uzoefu wa “Njoo uone”, au kujihusisha kwa njia nyingine na Nenda Kaskazini, tafadhali tuandikie kwa: info@maniafrica.com.

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us