Kundi la watu: wahamiaji wa Kachina wanaokuja Afrika
Katika Afrika yote, raia wa Kichina wanawasili kwa ajili ya kuja kufanya biashara. Wengi wamekuja kuwekeza na kupata pesa, ingawa wengine wameajiriwa na Wachina wengine kufanya kazi kama vibarua, wafanya kazi wa viwandani, au hata makahaba.
Uwepo wa watu wa China barani Afrika haujapokelewa vyema kote, huku wasiwasi ukiibuka juu ya matukio ya rushwa na wakati huo serikali za wenyeji zikiwezesha vitendo vya unyonyaji vinavyoathiri haki na ustawi wa weneyeji. Hata hivyo wanafika Afrika, kama watu wasio wa dini wanaomhitaji Yesu.
Watu wa China mara nyingi huwaona watu wa kidini kuwa ni watu wasio na mantiki na wasiofaa; hata hivyo, ushirikina kama vile nambari na rangi za bahati vimekamata sana fikra za Wachina. Ibada na mila zinazohusiana na mababu zina mizizi ndani ya utamaduni wao. Imani katika ulimwengu wa roho pia ni jambo la kawaida.
Watu wengi wa China wanaweza kuwa na mtazamo wa chuki dhidi ya Waafrika, lakini bado wanaweza kufikiwa na Waafrika kwa injili. Kwa wengi, Wakristo wanaokutana nao katika Afrika wanaweza kuwa ndio pekee wanaokutana nao, na fadhila zetu zinaweza kufungua macho yao wauone upendo wa Mungu kwao.
KWA KIFUPI
- Idadi ya watu wa China ilikuwa bilioni 1.4 mwaka 2022. Kuna Wakristo wapatao milioni 28, wengi katika makanisa ya chinichini/siri.
- Uchina ni mojawapo ya nchi ambazo sio za kidini zaidi duniani, lakini watu wake bado wanajihusisha na mambo ya kishirikina na mambo ya kiroho.
- Kambi za vijana, Shule za Jumapili, na njia zingine za kuwafikia vijana zimepigwa marufuku. Katika baadhi ya mikoa, watoto hawaruhusiwi kuhudhuria kanisani.
OMBA KWA AJILI YA
- Roho Mtakatifu kuwaonyesha Wachina kwamba hisia zao za kujiona wanajitosheleza ni za uongo, na kwamba wanamhitaji Yesu.
- Waafrika wanaoishi karibu na Wachina wamheshimu Mungu katika mitindo yao ya maisha na matendo yao ili Wachina waone tofauti.
- Watu wa Kiafrika wanaojifunza Kichina kwa ajili ya fursa za kibiashara ili waitwe na Mungu kuwafikia Wachina.
- Wachina wafunguke kuipokea injili.
Chanzo: Dk. Bi. Pauline Chiu Settles, mhamasishaji wa umisheni anayefanya kazi na shirika la USA Care Ministries International Mission Network News