Skip to content

🌍 First Parents Conference for African Missionary Kids 🌍

A parent shares what they discovered 👉 Read Here

Kutoa tangu mwanzo

Kanisa la Kale Heywet la Ethiopia lililoanzishwa mnamo mwaka wa 1927 (EKHC) lina takriban washirika milioni 12 katika Zaidi ya makusanyiko 12,000 ya mahali. Tangu kuanzishwa kwa kanisa, makusanyiko ya mahali yalitarajiwa kushirikisha injili mara tu walipoanza kumfuata Yesu, na kuliwezesha kanisa kutuma watu nje wakiwa na ujumbe wa Injili. Mchungaji Tesfaye Abadura, Mkurugenzi wa Umisheni wa kiulimwengu wa EKHC anasema, “Umisheni uko kwenye (Vinasa) DNA yetu.”

Dhehebu hilo, ambalo katika Kiamhari humaanisha “Neno la Uzima,” hutegemeza wamishenari na wenzi wao 38 wanaofanya kazi ndani ya Ethiopia na katika nchi ya Mali, Ghana, Nigeria Kaskazini, Sudan Kusini, Guinea, Kaskazini mwa Kenya, Somalia, na nchi nyinginezo za Afrika na Asia. Wanapanga kutuma watenda kazi Mashariki ya Kati na kwingineko, wakilenga Dirisha la 10/40.

Shirika la Injili

ECHC hufadhili shughuli zake za kimishenari kupitia Shirika la Injili. Kila mshirika wa kanisa anakuwa sehemu ya shirika hili na wanafamilia wanasajiliwa tangu kuzaliwa. EKHC inaamini kwamba huduma ya kwanza ya Kanisa ni umisheni daima; kwa hiyo, kila mshirika anapaswa kuchangia katika kueneza injili.

Katika nchi nzima, kwenye Meza ya Bwana ya kila mwezi, washirika huja na vitambulisho vya Shirika la Injili na sadaka zao kwa ajili ya umisheni. Makanisa mengine yana siku maalum za kufadhili, au hutumia likizo za Krismasi, Mwaka Mpya, au Pasaka kuchukua sadaka maalum. Makanisa pia hutuma sehemu ya zaka zao kwa ajili ya umisheni.

Utamaduni wa kufadhili

Sio tu makanisa makubwa ambayo yanatoa kwa ajili ya umisheni, pia. Wakati kanisa jipya linapoanzishwa, linatarajiwa kutuma na kufadhili mwinjilisti wa mahali hapo. Kanisa linapoendelea kukomaa, linapaswa kutuma wamishenari kwenye vikundi vya watu ambao hawajafikiwa karibu nao, na kulenga kutuma wamishenari duniani kote. Wamishenari hawa wa kimataifa wanachaguliwa na kutumwa katika ngazi ya kitaifa, ingawa hadi makanisa 10 yanaweza kushirikiana kumtegemeza mmisnhenari mmoja wa kimataifa. Baadhi ya viongozi wa wilaya wana kazi ya kutwa ya kusimamia programu za umisheni na utoaji katika makanisa yao ya kanda. Mchungaji Abadura anasema, “Inaanzia chini hadi juu.”

Kuhamasisha

Nchini Ethiopia, ni jambo lisilofaa kiutamaduni kwa mmishenari kujichangia au kuchangisha fedha kwa ajili yake mwenyewe; kwa hiyo, viongozi hufanya hiyo kazi. ECHC inawahimiza wachungaji kuhubiri kuhusu umisheni kila wiki. Kanuni tatu ndizo msingi wa mafundisho yao: kwanza, imani kwamba kusudi la Kanisa ni kufanya umisheni/utume ambao Yesu aliamuru. Pili, Mchungaji Abadura anauliza, “Tunaoneshaje upendo wa Mungu kwa wengine? Ikiwa hatuhubiri injili, basi hatumpendi Mungu wala kudhihirisha upendo wake.” Hatimaye ni kuharakisha kurudi kwa Kristo. Kulingana na 2 Petro 3:9, Kristo anataka kila mtu aifikie toba; kwa hiyo, wanajitahidi kadili wawezavyo kumpa kila mtu nafasi ya kumjua Yesu kabla hajarudi.

Mchungaji Abadura ana ushauri huu kwa madhehebu mengine ili kuona ongezeko la utoaji wao kwa ajili ya umisheni:

  • Fanya umisheni/utume kuwa huduma ya kwanza ya kanisa. Sio chaguo, lakini ni wajibu.
  • Hakikisha kuna timu ya maombi yenye nguvu yanayolenga umisheni, kwa sababu maombi hufungua mikono ya Mungu na mioyo ya watu.
  • Viongozi wa kanisa wanapaswa kuendelea kufundisha kuhusu utume/umisheni wa Mungu.
  • Umoja ni muhimu. Wakati makanisa yanapokuwa na umoja, kazi ya umisheni/utume inakuwa rahisi.
  • Fundisha kwamba Mungu huwapa thawabu wale watoao kwa ajili ya umisheni (Ufu. 22:12). Mungu ni mkarimu na tunapaswa kuwa wakarimu kwa kutoa kwa ajili ya umisheni
Other articles and resources from around the web on this topic:
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us