Mawazo ya kupata pesa ya kufadhili umisheni
Kitabu cha Tim Welch, New Funding Models for Global Mission, Learning From the Majority World, kinashirikisha njia za ubunifu za kufadhili misheni. Hapa kuna chache za kuonyesha jinsi ambavyo kila mtu anaweza kuchangia katika Agizo Kuu.
- Kikundi cha Kuanzisha Umisheni: Kundi la watu wanaoweka hai umisheni mbele ya kanisa la mahali kwa kushirikisha habari za umisheni, mahitaji ya kuombea, na kuhamasisha utoaji wa kifedha kwa ajili ya wamishenari.
- Kutenga vitu kwa ajili ya Umisheni: Washirika wa kanisa huteua sehemu ya kile walicho nacho kwa ajili ya umisheni, k.m., mauzo kutoka kwenye mayai yaliyotagwa na “kuku wa umisheni” aliyeteuliwa au faida kutokana na mauzo yaliyofanywa katika “siku maalum ya juma.” Kanisa linaweza pia kuendesha biashara ya teksi na kutoa faida yake kwa ajili ya umisheni.
- Mfano wa Kanisa Kumi na Mbili: Kanisa la mtaa linashirikiana na makanisa mengine 11 na kila mwezi, kanisa moja hutoa tegemeza ya kila mwezi kwa familia ya mmishenari.
- Mchele kidogo: Iliyotumika kwa zaidi ya miaka 100 nchini India, wanawake wa kanisa walitenga kiasi cha mchele kwa kila muda walipochambua kwa ajili ya kupika ili kutumwa kanisani na hatimaye kuuzwa ili kufadhili umisheni. Vitu vingine pia vinaweza kutumika.
- Kampeni za Ahadi za Umisheni: Washirika wa kanisa au familia wanaotaka kuunga mkono umisheni wanamwomba Mungu awasaidie kujua ni kiasi gani cha fedha cha kuweka ahadi. Kisha wanatoa michango mara kwa mara hadi ahadi kamili ikamilike.
- Akiba inayozunguka: Kila wiki, kiasi cha pesa kinatolewa kutoka kwenye matoleo ya kawaida na kuwekwa kwenye “sanduku la pesa” la umisheni ili itolewe mwishoni mwa mwezi.
- Shughuli na Matukio: Makanisa yanaweza kuandaa matamasha ya muziki, mashindano ya maswali ya umisheni, huduma za usafi, n.k. na kutoa mapato kwa ajili ya umisheni.