Barua kwa kanisa la Afrika
Sampson Dorkunor
Ikiwa umisheni ndiyo mapigo ya moyo wa Mungu, basi bajeti ya Kanisa lake lazima iakisi sawa katika ugawaji wa fedha. Hata hivyo, sivyo ilivyo, hasa katika Afrika.
Kufanya umisheni wa kuvuka utamaduni kuna gharama kubwa kama vile gharama za maisha, gharama za uendeshaji na gharama za maendeleo ya kimuundo. Acha tuchunguze gharama za maisha ya familia ya mmishenari yenye watu wanne wanaotumika Afrika. Baadhi ya mashirika ya kimisheni kutoka Asia yanahitaji mapato ya kila mwezi ya $2,300 hadi $2,500. Je, hii inalinganishwa vipi na mmishenari wa kiasili wa Kiafrika anayehudumu katika utamaduni mwingine?
Uchunguzi unaonyesha kwamba kiongozi wa umisheni wa Ghana, kwa mfano, anapokea kati ya $300 na $500, huku baadhi ya wamishenari walioko shambani wakipokea kati ya $100 na $200 kwa mwezi. Wengine hupokea kama $50 kwa mwezi. Zaidi ya hayo, Mwafrika wa kawaida ana jukumu la kuwasaidia wazazi wake wazee na washirika wengine wenye uhitaji. Maandiko yanauliza swali la kejeli: ni nani aendaye vitani kwa gharama yake mwenyewe (1 Kor 9:7-10)?
Dhana potofu
Ingawa wengine wanafikiri kwamba ufadhili wa umisheni wa Afrika lazima utoke kwenye vyanzo vya nje, kuna sababu za kutosha za kuamini kwamba Mungu hutoa ufadhili kwa ajili ya kazi yake katika Afrika.
Ingawa Mungu analiona kanisa la mahali kama ndo tegemeo la umisheni, inaonekana kuna tofauti kati ya mashirika yanayofanya kazi ya Mungu yasiyo makanisa na makanisa ya mahali. Mara nyingi, swali lisiloulizwa ni: “Kwa nini mimi, kiongozi wa kanisa la mahali, nikaunge mkono, kazi ya kiongozi wa shirika linalofanya kazi ya Mungu ambalo sio Kanisa?” Tunaonekana kusahau kwamba Ufalme wa Mungu ndio hatima katika kazi ya umishenari (Mt 24:14).
Wito kwa Kanisa la Afrika
Tuna wajibu wa kiuwakili kusaidia ufadhili wa umisheni wa Mungu duniani kote. Kanisa barani Afrika lina utajiri wa nguvu kazi, ujuzi wa kimishenari, na fedha. Suala ni jinsi ya kushirikiana na kuzipata pesa.
- Kanisa la Kiafrika lazima lihamasishe kutokea kwenye idara ya watoto kupitia uhamasishaji unaoleta uelewa wa umisheni. Wacha tuwapeleke watoto kwenye kambi za umisheni ili wajifunze kuomba, kutoa, kutuma na kwenda.
- Kuimarisha uhamasishaji wa wanafunzi wa vyuo vikuu na wahitimu kwa ajili ya safari za kimisheni. Kitu chenye nguvu ni kufanya ufuasi wa kimkakati ili kukiandaa kizazi kipya.
- Vijana wa Kikristo wa Kiafrika walioko ughaibuni wana jukumu la kutuma pesa nyingi barani Afrika. Fursa hii inahitaji kutumika ili kusaidia umisheni.
- Biashara za Kikristo za Kiafrika zinazofanya vizuri lazima ziwezeshwe ili kutumia biashara zao kama njia za kuwainua na kuwaachilia wanafunzi. Biashara za Kikristo huongezeka maradufu kama wafadhili wa injili ikiwa watafurahia kufadhili umisheni.
- Kuzingatia viwango vya uwajibikaji kwa fedha zilizopokelewa na kutumika ni muhimu.
Kwa Kanisa la Kiafrika kufikia malengo haya, mahubiri thabiti endelevu kutoka kwenye mimbari ni muhimu. Hii husaidia katika kuinua maombi, kuwawezesha Wakristo kwenda, kutoa, na pia kutuma wamishenari. Hatupaswi kukata tamaa kuzungumza juu ya milango hii iliyofunguliwa ya kushirikiana na Mungu.
Mtume Sampson Dorkunor ni Mwangalizi Mkuu, Living Bread Mission; Mkurugenzi, Kuwafikia Wasiofikiwa