Ubia kati a Mungu na mwanadam
Tshepang Basupi
Ongea na wamishenari wa Kiafrika na watakuambia kuwa changamoto yao kubwa ni pesa. Ninajua wamishenari kadhaa ambao waliacha wito huu kwa sababu ya ukosefu wa pesa kwa miaka mingi. Je, wamishenari Waafrika hawapaswi kufurahia baraka za ufadhili wa kutosha kama wamishenari wengine wanavyofanya? Je, Mungu hatakiwi kuwafadhili watumishi hawa waaminifu? Kwa nini wamishenari wanakosa pesa wakati wako katikati ya wito wa Mungu? Jibu labda ni kwa sababu kwa miaka mingi hatukuwahi kujiona kama wamishenari. Sasa kwa kuwa wamishenari wa Kiafrika wameibuka, makanisa yote barani hayajui jinsi ya kuwaunga mkono.
Suala la kuamini
Nilipohisi Mungu akiniita kuwa mmishenari, nilianza kujiandaa kujifunza kumwamini Mungu kwa sababu kuwa mmishenari kungehitaji kumwamini Mungu kwa wingi. Siku moja, nilimwomba Mungu kiasi kinacholingana na $20. Jioni hiyo, ndugu ambaye hakujua lolote kuhusu sala yangu alinipa kiasi kilekile. Alisema Mungu alimwambia anipe. Hiyo ilianza safari yangu ya kumwamini na kumwona Mungu akinipa mahitaji kwa mtindo kama huo kwa miaka 15 iliyopita.
Maandiko yana mifano mingi ya utoaji wa Mungu. Katika Kutoka 16, Mungu alitoa mana na kware kwa Waisraeli. Katika 1 Wafalme 17, Mungu alituma kunguru kupeleka mkate na nyama kwa Eliya. Je, hii inatosha? Je, maombi ndiyo pekee yanayohitajika?
Maandiko yana mifano mingi ya utoaji wa Mungu
Kushirikisha habari Pia mimi huomba na kushirikisha mahitaji yangu kupitia vijarida na mazungumzo na watu, na kisha Mungu huwahimiza kutoa. Nimefurahia ufadhili wa ajabu wa Mungu kupitia njia hii. Biblia inanena wakati ambapo Paulo anaandika barua kwa makanisa mbalimbali na kushirikisha mahitaji yake. Anaandika, “Ninapanga kwenda Hispania, na nitakapoanza safari, nitapita Rumi. Na baada ya kufurahia ushirika wenu kwa muda kidogo, mwaweza kufadhili safari yangu.” (Warumi 15:24).
Marafiki, familia, na taaluma
Wamishenari pia huomba msaada kutoka kwa marafiki na familia kwa ajili ya umisheni waliokusudia. Njia hii inategemea kuwa na jumuiya iliyojaliwa rasilimali kwa ajili ya shughuli hii. Jumuiya lazima pia ishawishike kuwa umisheni unafaa uwekezaji wao. Nimekuwa nikiomba msaada kwa miaka mingi na wale ambao wameshirikiana nasi walielewa umisheni na walitaka kuwa sehemu ya kile ambacho Mungu alikuwa anafanya kupitia sisi.
Wamishenari wengi hutumia miito yao na kulipwa wanapohudumu. Wengine walio na vipawa katika biashara huinua hiyo kama jukwaa la huduma na utoaji kwa familia zao. Njia ni tofauti, lakini ni muhimu kufanya kile kinachofanya kazi katika muktadha fulani.
Kutoa ni nafasi ya upendeleo Umisheni ni wa Mungu, na kwa hiyo ni wajibu wake kuwapa mahitaji wale wanaokwenda. Mungu anawataka waamini wote kushiriki katika kazi hii takatifu na ya ajabu ya kuunga mkono utume wake. Ni kazi ya wote matajiri na maskini pia, na ni fursa nzuri kushirikiana na Mungu katika utume wake wa kiulimwengu. Kama wamishenari, tunahitaji kufundisha na kushirikisha kikamilifu kuhusu umisheni katika jumuiya zetu. Kila fursa ya kuchagisha pesa ni fursa ya kusema kusudi la Mungu la kuwapatanisha wanadamu na yeye mwenyewe. Ikiwa watu wataweza kukubaliana na kile ambacho Mungu anafanya kupitia wewe, basi kuna uwezekano wataunga mkono.
Tshepang Basupi anahudumu kama Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Kusini na AIM International. Ameoana na Queen, na wana watoto wawili. Kwa sasa wako Johannesburg, Afrika Kusini.