Kufadhili umisheni katika Afrika
Duncan Olumbe
Bongo, mke wake, na watoto wake watano wanatumika kama wamishenari katika maeneo ya mbali ya kaskazini-magharibi mwa Kenya. Alitambua kwamba Mungu kweli anainua wamishenari kutoka Afrika. Wengi walikuwa wakienda kwa imani na huku wakipata msaada mdogo wa kifedha. Bongo anajua, hata hivyo, kwamba kufadhili umisheni bado ni changamoto kubwa. Wamishenari wengi wa Kiafrika kama yeye walikuwa wametumwa na “kutelekezwa” kwenye shamba la umisheni huku wakiwa hawana rasilimali za kutosha. Sababu mbalimbali zinahusika kwa hili—ukosefu wa ufahamu wa Kibiblia, Mazoea ya kihistoria, uwakili wa rasilimali, na hali halisi ya sasa ya utumaji.
Msingi wa kibiblia wa uwakili wa rasilimali na wa kifedha ndio sehemu ya kwanza katika kujenga theolojia thabiti ya kufadhili umisheni. Hii inatulazimisha kuchunguza vifungu kama vile “Nenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha uje, unifuate” (Mt. 19:21; Mk. 10:21, wanawake waliofadhili huduma ya Yesu (Lk. 8:1-3 ), kazi ya kutengeneza mahema ya Paulo (Mdo. 18:1-4) na mifano kujitafutia ufadhili(Flp. 1:3-6), na uwakili wa kibiblia kwa ujumla (Lk. 6:38).
Kihistoria, Kanisa la Kiafrika limejitahidi kuvunja pingu za ugonjwa wa utegemezi: “Sisi ni maskini na hatuwezi kufanya mengi,” “ni wazungu matajiri pekee ndio wanaoweza kufadhili umisheni.” Hili linaambatana na upendeleo wa ubaba ambao hauwawezeshi Waafrika, na mchezo wa kimamlaka wa wale walio na hali nzuri zaidi kiuchumi ambao hupenda kufuata “mtazamo wa kimasihi.”
Tuishi kwa urahisi ili wengine waweze kuishi.
Mitazamo hii imeathiri jinsi tunavyoitazama pesa na umisheni barani Afrika. Kwenye kiini ni mtazamo wa kujiona duni. Zaidi ya hayo, mitego ya kupenda mali na ulaji wa mali inajitokeza miongoni mwa tabaka la kati linalokua la Afrika. Changamoto ni jinsi ya kupata uwiano kati ya shauku yetu ya kuepuka umaskini na mafundisho ya Biblia ya “utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa” (1 Tim. 6:6)
Bongo alitafakari: Ingawa mtindo wa kutafuta watu wa kukufadhili wa Magharibi umesababisha kutumwa kwa wamishenari wengi, yawezekana kwamba sisi pia kama wamishenari wa Kiafrika na watumaji wa wamishenari tunahitaji kupata mifano inayofaa zaidi kulingana na hali halisi ya Kiafrika?
Akiutazama wakati ujazo kwa matumaini, Bongo aliomba kwa ajili ya mwitikio uliokitwa katika theolojia ya kibiblia ya jumuiya na ukarimu. Kiutendaji, tunahitaji kuzingatia zaidi uwakili wa kibiblia, matumizi endelevu ya rasilimali za Mungu pamoja na uwajibikaji kwa Mungu na wanadamu (Rum. 14:12; Gal. 6:1-2), na mtazamo wa muda mrefu wa kufadhili umisheni kibunifu na sera nzuri za mazingira na kijamii. Kinabii, tunahitaji kustawisha ukarimu kutoka kwenye umaskini wetu (2 Kor. 8:1-3) na kuishi maisha rahisi zaidi (Ayubu 1:21). Ni lazima “tuishi kwa urahisi ili wengine waweze kuishi” (Ron Sider).
Katika toleo hili la AfriTWENDE, tiwa changamoto kutokana na kujitoa kwa Baba Akawu kwa ajili ya kufadhili umisheni licha ya hali yake. Katika makala yetu ya Mtazamo, Tshepang Basupi anatushirikisha mbinu mabalimbali za kupata pesa kwa ajili ya umisheni. Hadithi yetu ya Makala inaangazia uzoefu wa ufadhili wa CAPRO kama shirika la kimisheni la Kiafrika na inaonyesha uaminifu wa Mungu katika kufadhili kazi yake. Furahia kusoma na washirikishe na wengine!!
Duncan Olumbe ni kiongozi wa umisheni wa Kenya, mhamasishaji wa maendeleo ya jamii, mkulima wa kilimo hai, mtetezi wa utunzaji wa uumbaji, na mpanda milima wa karibu miaka 30 ya huduma katika mataifa mbalimbali. Ana uzoefu katika umisheni wa kuvuka tamaduni na huduma ya wanafunzi. Anahudumu kama Mkurugenzi wa Kanda wa Interserve International, na Mkurugenzi Mtendaji wa Peer Team Kenya. Amemuoa Roseline na wamebarikiwa vijana watatu wa kiume. Anaweza kupatikana kwa duncan.olumbe@gmail.com