Skip to content

“Kutoka Nigeria hadi Malawi” – nyakati za wamishenari

Bolaji Sholoton, mmishenari nchini Malawi
Nilizaliwa katika familia ya Kiislamu ya kawaida, na mara kwa mara nilikuwa nikifuatana na marafiki zangu kwenda kwenye makanisa yao. Nilipata fursa nyingi za kuwa Mkristo, lakini sikutaka.
Kila mwaka mpya nilikuwa nikijiwekea azimio la kumkaribia Mungu zaidi. Hata hivyo, azimio hilo halikudumu hadi mwisho wa Februari.
Mwishoni mwa mwaka 1997, niliamua kwamba sitaki tena kuwa na maazimio ya Mwaka Mpya ambayo hudumu kwa muda mfupi. Usiku wa kuamkia Krismasi, nilienda katika kanisa nililolifahamu na nikayatoa maisha yangu kwa Kristo.
Marafiki zangu waliendelea kunifuatilia na kunitia moyo ili kuhakikisha kwamba siondoki katika imani.
Baada ya kuokoka, mmishenari mmoja alikuja kanisani kwetu kuhamasisha watu kuhusu umisheni na akatupatia kaseti zilizokuwa zikizungumzia kazi ya umisheni.
Nilisikiliza kaseti hizo kwa muda wa miezi sita, na nikatambua kwamba hiki ndicho nilichotaka kukifanya katika maisha yangu.
Leo hii, mimi ni mmishenari ninayewaonyesha wengine jinsi ambavyo wao pia wanaweza kuwa watoto wa Mungu.
Soma simulizi kamili hapa: