“Kuwafikishia Wayao Injili” – nyakati za wamishenari

Henry na Annie Bisani, wamishenari miongoni mwa Wayao mpakani mwa Msumbiji na Malawi
Nilizaliwa katika familia ya Kikristo, lakini sikuokoka hadi nilipokuwa kijana, baada ya kuhudhuria mkutano wa wazi wa injili. Nilikuwa na shauku kubwa ya kujifunza zaidi kuhusu Bwana ili niweze kuhudumu katika kanisa langu.
Nilihudhuria mafunzo yaliyoandaliwa na Teen Missions. Shule ya mafunzo ilikuwa katika eneo la Wayao. Moyo wangu ulihisi huzuni nilipoona kwamba hawakumjua Bwana Yesu. Tangu wakati huo sikuwa tena na hamu ya kurudi katika kanisa langu lililojaa Wakristo -jina tu.
Nilirudi nyumbani nikiomba Mungu anipe shirika ambalo lingenisaidia kuhudumu miongoni mwa Wayao. Mungu akaniunganisha na CAPRO, ambayo tayari ilikuwa ikifanya kazi miongoni mwa Wayao. Walinituma katika moja ya vituo vyao vya huduma. Hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kujifunza lugha na utamaduni wa Wayao.
Watoto wadogo walifurahia jitihada zangu za kujifunza lugha yao na walikuwa wakikusanyika nyumbani kwetu mara kwa mara. Watoto hao wakawa daraja letu la kwanza la kuifikia jamii nzima.
Mke wangu alijiunga nami mwezi Januari mwaka 2016, jambo lililokuwa hatua kubwa katika huduma yetu. Kwa sasa tuna kanisa lenye washiriki sita, akiwemo mke wangu na mimi. Tulijifunza lugha yao kupitia wao, na tukawafundisha simulizi za Biblia kwa kutumia lugha ya taifa.
Soma simulizi kamili kwa kiingereza hapa: