Skip to content

“Baba yangu hakuwa Mkristo” – nyakati za wamishenari

Musa Lazari, mmishenari nchini Tanzania
Mama yangu alikuwa Mkristo, lakini baba yangu hakuwa Mkristo. Kukulia katika familia ya namna hiyo kulikuwa changamoto, lakini mama yangu alifanya kuwa lengo la maisha yake kunifundisha kuhusu Yesu. Shauku hiyo kwa Yesu ilichochewa zaidi na mwalimu wangu wa Shule ya Jumapili.
Siku moja mwaka 1981, nilienda kanisani, na mchungaji akauliza kama kuna yeyote aliyependa kumpokea Yesu. Siku hiyo niliokoka.
Nilikuwa na hamu ya kumfuata Yesu. Nilienda Chuo cha Biblia Katungulu huko Mwanza, na baadaye Chuo cha Theolojia cha Nassa. Nikiwa katika shule ya Biblia, kwa mara ya kwanza nilisikia kuhusu makundi ya watu ambao hawajafikiwa na huduma za umishenari za kuvuka kwenda tamaduni nyingine.
Kwa sasa ninahudumu kama mmishenari miongoni mwa Waswahili katika Pwani ya Kusini ya Tanzania. Nafanya kazi na Africa Inland Church Tanzania. Sasa nina zaidi ya miaka 20 katika huduma ya umishenari.
Somo kubwa zaidi nililojifunza ni umuhimu wa kujua lugha ya watu unaowahudumia. Hii ni mojawapo ya njia bora za kuwafikia watu. Ukiweza kuzungumza lugha yao, unaweza kuzungumza na mioyo yao.