Skip to content

“Kuponywa kwa ajili ya kutumikia”

MATILDA NTUKELA: Kutoka Afrika Kusini hadi kwa Wamalagasy nchini Madagascar
Safari yangu ya imani ilianza mwaka 1994 wakati nilipoelezwa habari za Yesu kwa uwazi kupitia hadithi ya mwanamke aliyekuwa na tatizo la kutokwa damu. Nilijiona katika yule mwanamke kwa sababu nami nilikuwa na ugonjwa uliotumia akiba yote ya mama yangu tulipokuwa tukizunguka kwa madaktari na waganga wa kienyeji. Niliokoka, na nilifurahia kuwasaidia wengine wamjue Yesu huyu.
Nilijitolea kwa muda wa wiki mbili katika meli ya Operation Mobilisation (OM) ya Doulos, na hapo ndipo niligundua umishenari kwa mara ya kwanza. Niliona watu wengi waliokuwa wameacha familia zao na kuzunguka wakishiriki upendo wa Mungu. Niliguswa sana na nikahamasika kujitoa kama wao.
Meli ilipotembelea kisiwa cha Madagascar, jambo la ajabu lilinitokea. Nilihisi upendo mkubwa kila nilipowakaribisha Wamalagasy ndani ya meli, na nikajenga mahusiano na baadhi yao.
Mwisho wa mwaka 2007, Africa Inland Mission (AIM) walinialika kwenda kufanya kazi Madagascar. Walihitaji hasa mwanamke wa kuwafikia wasichana na wanawake. Niliomba kuhusu hilo na hatimaye nikaungana na AIM, nikahamia Antananarivo mwaka 2013.
Soma hadithi kamili kwa kiingereza hapa: https://afrigo.org/…/missionary-profile-matilda-ntukela/
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us