“Kutoka kukataa umishenari hadi mhamasishaji”
Mara tu baada ya kumaliza shule ya sekondari, mchungaji wangu ambaye ni mkurugenzi wa Operation Mobilization alionekana kuona “mmishenari” ndani yangu. Nilicheka na kusema, “kamwe haiwezekani!” Nilikuwa nataka kwenda chuo kikuu, si kukaa kwenye vibanda vya udongo na kuhubiri. Alinipa siku tatu za kuomba. Sikupanga kufanya hivyo, lakini kwa siku tatu bila usingizi usiku, waliopotea/hawajaokolewa walinisumbua mawazoni hadi nikajisalimisha.Miaka kadhaa kabla ya hapo, nilikuwa nimemjua Yesu katikati ya familia iliyovunjika. Mama yangu wa kambo, aliyekuwa akijihusisha na uchawi, ulevi na uvutaji sigara, karibu apoteze maisha; alipoacha mambo hayo na kurudi kanisani, nami niliokoka kwa mabadiliko makubwa.
Wakati wa mafunzo ya umishenari, nilihubiri katika kijiji kwa wiki moja, maisha yalibadilika kwa namna ya ajabu. Nikagundua kwamba kama Yesu angerudi wakati huo, kijiji kile kingekuwa tayari, lakini familia yangu haikuwa tayari. Nilimsihi Mungu awaokoe, nikiahidi kumtumikia maisha yangu yote. Siku chache baadaye, jamaa zangu wote walilia na kumpokea Kristo.
Nilihudumu kusini mwa Afrika, nikasoma theolojia nchini Brazil kwa miaka minne, na hata kuongoza kituo cha mafunzo huko. Hata hivyo, Msumbiji iliendelea kunivuta kurudi. Sasa nimerudi nyumbani, nikihamasisha makanisa ya mahali hapa kuacha kuomba tu na badala yake waende. Tumenunua ardhi kwa ajili ya shule ya kwanza ya kitaifa ya umishenari nchini Msumbiji.
Soma hadithi kamili kwa kiingereza hapa: https://afrigo.org/stor…/missionary-profile-estevao-gomes/