Skip to content

“Nilijaribu karibu kila dini” – nyakati za wamishenari

Nilikuwa sina utulivu. Moyoni mwangu, nilijua kwamba nilikosa amani, hivyo nikaamua kuitafuta kila mahali. Nilikuwa Mkatoliki, lakini sikuipata amani huko. Mama yangu hapo awali alikuwa Mwislamu kabla ya kujiunga na baba yangu katika Ukatoliki, kwa hiyo nilienda kwenye dini yake kuona kama moyo wangu ungepata pumziko. Haukupata.
 
Niliachana na imani hiyo na kujiunga na Mashahidi wa Yehova, kisha nikaacha. Niliingia katika Ufumbo wa Mashariki (Eastern Mysticism) uliyoniahidi amani niliyokuwa nakiitamani. Hata hivyo nikaacha. Baadaye nikawa mtu wa kushikilia sheria sana (legalist) na kujaribu kufanya mema kwa nguvu zangu mwenyewe. Bado nilikuwa na huzuni na mtupu moyoni. Nikaacha.
 
Nilitambulishwa kwenye kanisa la sayansi, na licha ya “ukweli” wote niliokuwa nikiambiwa, bado nilikuwa mtupu kabisa ndani yangu. Ndipo nikaamua kwamba haistahili tena. Kwangu mimi, Mungu hakuwa halisi tena. Hivyo nikawa mpagani (atheist).
Nilikuwa mpagani (atheist) mwenye sauti kubwa na mwenye kubishana sana. Mimi pamoja na kikundi cha vijana wengine wanne tulifanya kupinga uwepo wa Mungu kuwa lengo kuu la maisha yetu; tulijiona kuwa wenye hekima sana.
 
Siku moja, tulisikia kuwa kulikuwa na mkutano wa Injili uliopangwa kufanyika katika Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya. Tukiwa tumejizatiti kwa hoja na hoja za kupinga, tulikwenda kama kwenye vita.
Mara tu tulipofika langoni, tulikutana na vijana ambao mara moja walianza kuzungumza nasi.
 
Mmoja alinichukua hadi kwenye hema lililokuwa ndani, kisha akanihubiria Neno la Mungu. Haikuchukua muda mrefu nikavutiwa na ukweli huu mpya ambao nilikuwa nimetumia muda mwingi sana kuupinga. Nikawa Mkristo.
Nilipata amani niliyokuwa nikiitafuta kwa miaka mingi! Nilikuwa kiumbe kipya, nami nilitamani kuwaeleza watu ukweli huu mpya, hasa Waislamu, kwa kuwa familia ya mama yangu bado ilikuwa imejikita sana katika Uislamu. Hivyo ndivyo nilivyokuwa mmishenari.
Mahali pa kwanza nilipoenda kupeleka Injili ya Yesu Kristo ilikuwa nyumbani kwa ndugu zangu. Lakini nilipitia pigo kubwa sana—baba yangu, ambaye hakuwa hata ameonyesha wasiwasi nilipokuwa nikizunguka katika dini nyingine zote, alinikana.
Sasa mimi ni mmishenari wa nchi za Kenya, Tanzania, na Ethiopia chini ya CAPRO.
 
Soma hadithi yote kwa Kiingereza kupitia https://afrigo.org/story…/missionary-profile-swahib-fathi/
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us