“Fanya uamuzi wa hatua inayofuata” – nyakati za wamishenari
Mwishoni mwa masomo yangu katika Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) nchini Kenya, nilihudhuria kozi ya uhamasishaji wa kimisheni ya Kairos (www.kairoscourse.org). Kwa mara ya kwanza maishani mwangu, nilitambua kuwa utume si kwa wachache tu—ni wito kwa kila muumini, nami nikiwemo.Mnamo mwaka 2017, niliondoka Afrika Mashariki kwa mara ya kwanza kwenda kuhudumu Uingereza, nchi ya wamishenari walioleta injili Kenya kwa mara ya kwanza!
Nilisaidia katika kuwafikia wahamiaji, kazi za vijana na watoto, kuwa rafiki kwa wanawake wasioamini katika jamii, na kufanya kazi mbalimbali za jumla kanisani.
Sisi wote tukiwa ni wageni, tulihisi umoja, na ilikuwa rahisi kwangu kuwafikia wahamiaji. Nilipata kushiriki na Wasyria, Warusi, na Wahindi. Nilikuwa daraja kati yao na kanisa la hapa. Nilipanga mikutano ya marafiki na jumuiya ya kimataifa na kuwasaidia kuungana na kanisa la hapa.
Ushauri wangu kwa vijana ni huu: hudumu na kutumika tangu utotoni/mdogo — unapo kuwa mdogo kabisa, ni rahisi zaidi. Huna mambo mengi ya kufikiria na watu ni wachache tu wa kuwaacha nyuma. Usihisi lazima ufanye uamuzi wa miaka 50 ijayo; fanya uamuzi wa hatua inayofuata tu na umwachie Bwana akuongoze.
Soma hadithi nzima kwa Kiingereza kupitia hapa https://afrigo.org/…/missionary-profile-daphne-kabeberi/