Skip to content

Watoto wa wamishenari wa Afrika mashariki

Worku Hailemariam

Wongel Mulugeta Wongel  (Injili) Zeleke, William Cary, Ephrem Getachew – haya ni majina ya baadhi ya watoto wa wamishenari wetu (WWW) ambao wanawakilisha ujumbe wa injili na maisha ya wamishenari. Kupitia majina ya watoto wao, wamishenari wetu hukumbushwa juu ya wito wao.

Kuandaa familia na watoto wao kwa ajili ya maeneo mapya huwa na changamoto. Ni muhimu kwa kanisa linalokutuma na misheni kufanya kazi pamoja kwa karibu kwenye maandalizi, ikiwa ni pamoja na matarajio juu ya changamoto zitakazokuja na jinsi ya kuzishughulikia kwa pamoja. Kwa njia hii, baadhi ya matatizo yanaweza kupungua. Kama ilivyo, familia za wamishenari na WWW ambazo tunakabiriwa na changamoto kwa pande zote mbili katika kipindi cha kutumwa na kupokelewa – changamoto ambazo ni za kihisia, kifedha, na kijamii.

Lugha

WWW wa Kiafrika kwa kawaida wanatarajiwa kuzungumza angalau lugha tatu. WWW kutoka katika muktadha wetu wa Kiethiopia huzungumza Kiamhariki, lugha yetu ya kitaifa. Aidha, wanajifunza lugha ya asili ya wazazi wao; lugha ya kimataifa kama vile Kiingereza, Kifaransa, au Kiarabu; na hatimaye, lugha ya kitaifa ya nchi ya utumishi, kama vile Kiurdu au Kichina. Katika hali nyingine, lugha ya asili kutoka nchi ya huduma pia huongezwa.   Mara nyingi wazazi hupendelea kutumia lugha zao ya asili za kikabila baina yao lakini hutumia Kiingereza au lugha ya huduma ya eneo husika kwa watoto wao. Hata hivyo, kuna wengine wanapendelea kuwafundisha watoto wao lugha ya asili ya wazazi wao.

Kwa upande mmoja, watoto walio katika mazingira ya kuzungumza lugha tatu au zaidi wakati wa miaka yao ya awali watapata lugha za ziada kwa urahisi zaidi. Kwa upande mwingine, kwa muda mfupi, uwepo wa lugha nyingi unaweza sababisha watoto kuchelewa kupata elimu kwa sababu ujuzi wa lugha ya elimu inayotakiwa  unakua bado haujakamilika.

Changamoto za Kiutamaduni

Kila mmishenari anatarajia kuishi katika utamaduni wa kigeni, lakini utamaduni mchanganyiko wa jamii ya wamishenari wa mataifa mengi unaweza kuwa wenye kushangaza. Baadhi ya maeneo, watoto hujiunga na jamii mbalimbali bila ufahamu wa makundi madogo au makubwa ya tamaduni. Hata hivyo, katika maeneo mengi WWW wa Kiafrika ni kundi la wachache kikabila na kitamaduni.  Katika kutilia mkazo  hili kunaweza pelekea  upweke na kujitenga, kama ambavyo WWW walivyosema  wakati familia yao iliporudi kwenye nchi yao kwa ‘majukumu ya nyumbani, “Tungetamani kubakia kwenye nchi yetu ili kuweza kuwa na marafiki wengi.”

Wakati familia zinapotengana, watoto wanaweza kuhisi kutelekezwa, na hata kuwa na uchungu kwa BWANA kwa kuchukua wazazi wao. Mzazi anaweza kufanya nini?

Elimu

Ukosefu wa fedha daima ni suala lenye changamoto kubwa sana pia kwenye elimu ya watoto. Matarajio ya kawaida ya kanisa linalotuma na jamaa ya wamishenari ni kwamba WWW wataweza kupata elimu bora zaidi nje ya nchi yao. Wanadhani popote pale misheni itakapokua inahudumia, shule nzuri zitakuwepo. Hata hivyo, huu sio uhalisia kila wakati. Dhana ya pili kutoka kwa kanisa linalotuma ni kwamba gharama ya elimu ya watoto inaweza patiwa ufumbuzi. Hata hivyo, huu pia sio uhalisia.

Kwa upande mmoja, wamishenari wanahangaika kulipia elimu ya watoto wao; kwa upande mwingine, makanisa yanahangaika haswa kuongeza zaidi msaada wa kifedha. Matokeo yake, wazazi wamishenari hubeba mzigo wa ziada wa kutafuta njia za kuongeza ufadhili  kwa watoto wao, jitihada hizi zinaweza kusababisha wasiwasi na msongo wa mawazo.

Wamishenari wa Kiafrika hawajui juu ya shule za nyumbani na masomo ya nyumbani na pia hazitambuliwi katika nchi zao.

Kutelekezwa

Mara nyingi, watoto wa wamishenari lazima kupelekwa shule, mara tu wanapokuwa wakubwa. Hii inaweza kuwa kwa sababu hakuna shule nzuri kwenye eneo husika, au wazazi hupendelea watoto wasome shule kwa lugha yao wenyewe. Au, masharti yanaweza kuwa magumu kwenye eneo ambalo wazazi wanatumika na wazazi huhisi watoto watakuwa huru zaidi mahali pengine. Wakati mwingine watoto huachwa kwenye nchi za nyumbani, pamoja na ndugu, kwa ajili ya shule.

Wakati familia zinapotengana, watoto wanaweza kuhisi kutelekezwa, na hata kuwa na uchungu kwa BWANA kwa kuchukua wazazi wao. Mzazi anaweza kufanya nini? Ni muhimu kwa wazazi kuwasiliana kwa uwazi na watoto wao kuhusu fursa na zipi zitakua  bora kwa muda mrefu. Uhusiano wenye na wa kusaidiana, unaweza kuwasaidia watoto kuhisi hawapelekwi mbali au kuachwa nyuma.

Mara baada ya mtoto kutenganishwa na mzazi, mawasiliano ya mara kwa mara ni muhimu na mtoto lazima ajisikie huru kuwashirikisha wazazi jambo lolote linalomtatiza. Ingawa ni rahisi kutingwa sana na huduma, kumbuka kwamba wewe kwanza ni mzazi na kazi ya pili ni mmishenari.

Licha ya gharama kubwa ya kufanya kazi ya umisheni haswa  kwa elimu ya watoto, ninaweza kushuhudia kwamba baadhi ya makanisa ya Kiafrika yanawasaidia wamishenari wao kwa kujitolea sana. Hawatoi msaada kulingana na “unafuu” ilivyo kwao. Badala yake, kama Paulo anavyosema katika 2 Wakorintho 8:3: “Maana nawashuhudia  kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao.’’ Nimeona kwamba baadhi ya makanisa yanayounga mkono huduma, japo majengo yao wenyewe kanisa yako katika hali duni na kuna vipaumbele vingine, yamejitolea kutoa kipaumbele cha kwanza kwa msaada wa mmishenari.

Haya yote yamesemwa, kwa kuwa tumefanya ziara za kimishenari kwa watu waliotumwa kutoka Ofisi yetu ya Afrika Mashariki, tumeona uwezo wa kushangaza na ustahimilivu wa WWW wetu. Wengine wanaweza kuwa marubani wamishenari, wahudumu wa tamaduni mchanganyiko, na walimu wa WWW wengine. Hili linatia moyo na tunaona kuwa tunaweza kuzalisha kizazi cha pili cha wamishenari.

Worku Hailemariam ni Mkurugenzi wa Ofisi ya SIM ya Afrika Mashariki huko Addis Ababa, Ethiopia, akihudumu kutoka 2012 hadi 2023. Ofisi hii inahamasisha, inaelekeza, na kuwatuma wamishenari kutoka Afrika Mashariki kuhudumu ulimwenguni kote. Makanisa ya Ethiopia yamekuwa yakituma wamishenari tangu miaka ya 1990.

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us