Skip to content

Safari yangu kama mama wa WWW

Mimi na mume wangu tuna wasichana wawili, Blessing na Joy. Wakati tulipokuwa tukijiandaa kuitikia wito wa Mungu wa umisheni wenye mchanganyiko wa tamaduni nchini Thailand, shirika letu lilituarifu kwamba eneo tulilopewa lilikuwa na mwalimu wa shule ya nyumbani kwa ajili ya watoto wa familia mbili, tayari alikuwa anahudumu huko. Tulitiwa moyo kwamba Baraka, aliyekuwa na umri wa miaka minane wakati huo, angeanda  pamoja nasi kwenda shambani mwa BWANA na kujiunga na kikundi hiki cha shule ya nyumbani. Baada ya kutafuta ushauri na maombi, tuliamua kwamba binti yetu mkubwa, Furaha, atakaa na ndugu katika nchi yetu ili kuanza masomo ya ngazi ya chuo kikuu. Ingawa kulikuwa na elimu ya chuo kikuu nchini Thailand, ilikuwa katika lugha ya wazawa.

Tuliwasili tukiwa tumejaa nguvu na muda mfupi badae  tulipata makazi nje ya mji. Ndani ya majuma kadhaa ya tangu tulipowasili, mwalimu wa shule ya nyumbani aliondoka. Hakukuwa na walimu wengine mahali pale.

Familia hizo mbili hivi baada ya muda mfupi ziliamua kuhamia tena kwenye mji mkuu ambapo kulikuwa na elimu yenye kiwango bora zaidi. Mimi na mume wangu, kwa haraka tukitimiza majukumu ya uongozi kwenye eneo letu la huduma, tuliendelea na maombi kwa kila machaguo yote ya kielimu ambayo  tuliyafikiri. Hatimaye familia nyingine ya wamishenari toka Afrika Magharibi iliwasil kwenye mji mwingine ulio umbali wa masaa manne kutoka kwetu. Tulipanga kuwa binti yetu, Blessing aende akaishi nao na kuhudhuria shule ya nyumbani kwenye mji huo, kwa bei nafuu na ni karibu kuliko mji mkuu.

Ninaweza kukwambia kwamba tulipomtafuta BWANA kwa bidii katika maombi, mambo haya mawili hayakua rahisi kuafikiana nayo kwa ajili ya binti zetu, Neema ya Mungu imekuwa kubwa kwetu, na ninaweza shuhudia kwamba wasichana wote wawili wanaendelea vizuri hivi leo. Hata hivyo, haikuwa safari iliyokosa changamoto.

Binti yetu mkubwa, Joy, alihisi kwamba kazi yetu ya umisheni ilikuwa “imetuiba” sisi kutoka kwake. Kuishi na ndugu yetu kulikuwa na shida sana kiasi kwamba ilimlazimu mume wangu kurudi nyumbani kusaidia kuitatua. Kipindi cha maisha ya ujana, wanapotoka nyumbani na kufikia hatua za awali za utu uzima kimejawa na vikwazo, hata kama ni kwenye mazingira mazuri. Miaka miwili baadaye wakati wa mgogoro nchini kwetu, shirika letu la umisheni  ilifanya bidii kumtunza na kumlinda binti yetu. Kupitia mwitikio wa misheni katika kipindi hiki cha hatari, Joy  alipata upendo wao mkubwa. Leo tunamsifu Mungu kwamba Joy ni msichana aliyefanikiwa.

Neema ya Mungu imekuwa kubwa kwetu, na ninaweza shuhudia kwamba wasichana wote wawili wanaendelea.

Na pia mpango wa Blessing ulikuwa mzuri kabisa, japo haukukosa changamoto. Tulimpa simu ili atupigie mara nyingi kadiri ilivyohitajika. Familia wenyeji walikuwa na ukarimu wa kweli na makini kwa mahitaji yake yote. Lakini familia ambayo si yako inawezaje kumwadhibu mtoto wa mtu mwingine pale ambapo hafanyi kazi za shule? Matokeo yake kitaaluma yaliathirika kwa namna fulani. Adha au aibu ni jambo lisiloepukika kwa mtoto anayeishi na familia nyingine. Hata alipopokelewa kwa  uchangamfu hatukuweza kumsaidia Baraka kutoka kwenye mawazo ya kuhisi pengine  labda wazazi wangu hawanitaki, hisia ambazo si za ukweli!!

Usiwe mwenye hofu kuukwepa wito wa Mungu wa umisheni. Malezi yana changamoto hata kama unakaa nyumbani.

Kama wazazi, hasa wazazi wa WWW, tunajifunza kila wakati. Acha nitoe baadhi ya kanuni tulizokusanya njiani:

    1. Washirikishe watoto wako kwenye majadiliano kuhusu mabadiliko yajayo, nini kitatokea, jinsi kitakavyotokea. Hata vijana wadogo wana hisia, mawazo na maoni. Waache waongee.
    2. Wasaidie watoto wako kupitia mabadiliko. Sio tu mtazamo wako mzuri, lakini pia waruhusu kuchukua kitu ambacho ni maalum au chenye kuwafariji, wape uhakika wa usalama popote watapokuwa.
    3. Panga mipango, tena na tena… na uwe tayari kwa mambo ya kushangaza. Licha ya mipango bora, timu za umisheni na rasilimali za misheni zinaweza kubadilika mwaka hadi mwaka. Machaguo yako ya mwaka mmoja huenda yasiwe sawa na ya mwaka ujao.
    4. Wakala wa umisheni na kanisa linalotuma lazima wajue vizuri juu ya shule za mahali watakapokwenda wamishenari. Haijalishi kazi fulani ni ya dharura au ya kimkakati kiasi gani, mahitaji ya watoto ni muhimu vile vile.
    5. Kuishi katika tamaduni mbalimbali kutawatengeneza, kutawastawisha na kuwachanganya wanao. Wasaidie kuelewa tofauti za tamaduni na kuwasaidia kujibu kwa ujasiri maoni toka kwenye familia yako, watu wa eneo lako, na wamishenari wa mataifa mengine. Mstari kwa ajili ya watoto wangu ulikuwa 1 Petro 3:15, “Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu;lakini kwa upole na kwa hofu”.

4.1 mk mum2

Usiwe mwenye hofu  kuukwepa wito wa Mungu wa umisheni. Malezi yana changamoto hata kama unakaa nyumbani. Kufuata mapenzi ya Mungu kwako na familia yako daima ni mahali na jambo sahihi kutenda. Mojawapo ya mistari ninayopenda ni Isaya 30:21 “na masikio yako yatasikia neno nyuma yako, likisema, Njia ni hii, ifuateni; mgeukapo kwenda mkono wa kulia, na mgeukapo kwenda mkono wa kushoto.“ Hii ndiyo njia; tembea katika njia hiyo.

Ikiwa tunatafuta hekima ya Mungu, panga vizuri, na kujitoa kwa watoto wetu wakati wa changamoto, basi tuna kila tumaini watakua watu wenye uelewa mzuri na ufahamu mzuri. Na Mungu atawaongoza katika majukumu ambayo malezi yao ya kipekee baadae hata yakiwa na changamoto utakuwa umewaandaa kitamaduni. Kama mwandishi mmoja alivyosema, “matuta ni yale wanayopanda juu yake.” Kwa msaada wako, watoto wako na wapande juu kwa ajili ya Mungu.

Changamoto za kipekee kwa Waafrika

Ndani ya Afrika, WWW wa Kiafrika mara nyingi “hufichwa” kwa sababu huwa wanachanganya. Wamishenari wengine na watu wa eneo hilo wanaweza wasifikirie kuwa wao ni WWW kwa sababu hawajazoea kuwaona Waafrika katika kazi na majukumu kama haya.

WWW wanaweza kuwa na changamoto kubwa za lugha kwa kuhitaji kujifunza lugha mama na lugha ya biashara ya wazazi wao, lugha ya wazawa pamoja na lugha ya biashara ya mahali ambapo wazazi wao wanahudumu, pamoja na lugha ya kujifunza  shuleni! Familia ya wazawa inaweza isijue jinsi ya kuwakubali kikamilifu WWW  wako ambao wamekuwa tofauti na binamu zao au marafiki wa nyumbani. Maneno yenye kumdhihaki mtoto wako kwa rejareja kwa kutozungumza lugha ya wazazi wake vizuri, kutokula kama wao, na kuelezea tofauti zingine. Hata kwa mzaha, maneno haya yanaweza kufikisha ujumbe hasi au wa hila kwa WWW kuhusu utofauti wao.

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us