Kufuatilia kwa makini mapito na mabadiliko ya Watoto Wako
Watoto wa wamishenari ni wahamaji (WWW). Huu ni uhalisia kwa watoto wa familia za kimishenari. WWW huacha nchi zao za asili ambazo kwazo kuna shangazi na wajomba zao, babu, binamu na marafiki na wanafunzi waliosoma pamoja, na kanisa lao lililowatuma. Huanza makazi katika nchi ya kigeni na baada ya muda fulani hutembelea tena nchi zao za asili. Wakati mwingine wazazi huhamishwa na kupewa eneo na huduma nyingine. Hata kwa WWW ambao wazazi wao hukaa katika eneo moja, wamishenari wengine wanaowazunguka wanaweza kuja na kuondoka, inamaanisha wanapaswa kuwakaribisha na kuwaaga mara kwa mara.
Mojawapo ya mbinu bora ambazo mzazi mmishenari anaweza kujifunza ni namna ya kuwaongoza watoto wao kupita katika mabadiliko, kuwaandaa kusema kwa heri kwa moyo wao wote na kubisha hodi kwa moyo wenye tumaini, na kuwa na utayari wa kuanza ukurasa mpya. Wazazi ambao wana ufahamu na busara wanaweza kusaidia kuendeleza ustahimilivu na ujuzi kwa watoto wao ambao ni pamoja na kuchukuliana na mazingira waliyopo na katika kufanya huduma vizuri kwenye maisha yao yote.
Hebu fikiria juu ya kijito kipana chenye kingo pande zote. Kwenye ukingo mmoja ni mahali ambapo mtoto wako anaishi kwa sasa, na kwenye ukingo wa mbali ni mahali atakapoishi baadaye. Maji yaliyopo katikati ni mapito ambayo yanaweza kupitiwa vibaya, vizuri au katika ustadi mzuri zaidi. Na kwa hivyo pale ambapo dhoruba zisizotarajiwa zikitokea na kufanya njia ya kupita iwe ngumu, kukiwa na mpango wa kuvuka ambao umefikiriwa vizuri utamsaidia mtoto kustawi vizuri hata kama kuna matukio vya kushangaza.
Waandishi wa kitabu kiitwacho ‘Third Culture Kids: Growing Up Among Worlds’ wanapendekeza hatua nne ambazo kila mtoto wa mmishenari anapaswa kupitia ili kujiandaa kihisia kwa maisha yake mapya. Hatua hizi huwasaidia wazazi kupanga mapito kwa kusudi la kuwaweka watoto wao wawe na muda wa kufikiri juu ya kile kinachokuja, huku wakiwa na uhakika wa kuagana vizuri na kuondoka kwa moyo mkunjufu na kwa njia bora. Hatua hizo nne ni upatanisho, uthibitisho, kuaga na kufikiri juu ya hatima.
Upatanisho
Upatanisho unahusu kuweka mambo sawa katika mahusiano ambayo yataachwa nyuma. Inamaanisha kukaa chini na kusuluhuhisha magonvi au migogoro yoyote na watu wengine. Kuomba au kutoa msamaha huondoa wasiwasi kwenye moyo wa mtoto na humuaandaa kuenenda katika mahusiano mapya kwenye makazi yajayo. Njia mbadala ambayo ni yenye majaribu ni kuyahifadhi matatizo ya eneo moja na kuyaacha nyuma. Hii haiwezi kukusaidia kwenye huduma; kwa sababu kila mmoja wetu anajipeleka mwenyewe na mazoea yake pamoja nasi katika maeneo mapya. Upatanisho ni jambo ambalo mtoto anaweza kulitumia katika maisha yake yote.
Uthibitisho
Uthibitisho unamaanisha hali ya kuonyesha thamani ya mahusiano muhimu ambayo yataachwa nyuma. Ni watu gani na kumbukumbu zipi zinaweza kuthibitishwa na kuthaminiwa? Je, ni nani ambaye wewe na watoto wako mnaweza kumshukuru kwa ushawishi na mchango wake kwenye familia yako? Hakikisha mnapiga picha pamoja, unaandika jumbe za shukrani, au kutoa zawadi maalumu ili kukumbukana. Hatua hii itamsaidia mtoto wako kukumbuka nyakati nzuri na watu wazuri kwa wakati mrefu ujao. Mchakato huu utamruhusu mtoto wako kupitia mabadiliko chanya.
Kwa Heri
Kwa heri ni kitendo cha kuagana. Inaweza kuonekana ni jambo la kawaida sana kulitaja, lakini katika harakati za kuwahi kuondoka, hupunguza nafasi ya watu kuagana vizuri na jambo hili huachwa mpaka dakika ya mwisho kabisa. Unapoharakisha kuaga huacha mambo mengi bila kusemwa na inaweza pelekea kuhisi kutoridhisha. Kuagana sio tu kwa watu maalum, lakini pia hata kwa maeneo kama vile shule yao au mgahawa pendwa, matukio au mila ambazo walizijua mara kwa mara, na hata kuaga vitu. Andaa orodha ya watu, maeneo uliyotembelea mara ya mwisho na ambayo yalikupa uzoefu na lipe nafasi jambo hili wiki chache kabla hujaondoka. Andaa sherehe ya kuwaaga marafiki wa mtoto wako. Mkiwa wazazi ambao hutingwa na majukumu mengi huku mkipanga hatua zijazo wanapanga kwa bidii hatua zinazofuata, kupakia mizigo, na kukamilisha kazi za huduma, hakikisha unachukua muda wa kuaga, panga tarehe kwenye kalenda. Kusema kwaheri kunaumiza lakini ni muhimu kufanya hivyo kabla ya kuchukua hatua nzuri kuelekea eneo linalofuata.
Fikiria juu ya ukomo wa Safari
Fikiria mahali unakoenda ina maanisha kujifunza na kuota ndoto juu ya eneo jipya. Hebu waza pamoja na watoto wako ni kwa namna gani itakavyokua mkifika huko. Fanya utafiti kwenye mtandao. Andika sifa nzuri za kuhamia eneo jipya na manufaa yatakayopatikana pamoja na mambo mtakayopata huko. Msaidie mtoto wako ajione kwenye mazingira mapya – katika shule mpya, nyumba mpya; chukua hatua kwa matendo kujiandaa kwa ajili yake. Ni sawa kujihisi kuwa na shauku juu ya eneo jipya na itakuwa ni vigumu kama unahisi huzuni kuliaga eneo unalolifahamu na ulilokua unalipenda. Ni muhimu kumwambia mtoto hivi kuwa ni lazima, ni sawa hata kwa wao kuwa na huzuni, haswa wakati kama huu kuna hisia tofauti tofauti huinuka juu ya jambo jipya linalokuja.
Imechukuliwa kwenye kitabu cha Third Culture Kids; Growing Up Among Worlds na Dave Pollock na Ruth Van Reken.
Maswali 9 ya kujiuliza kabla ya kuondoka
- Umri: Watoto wako wana umri gani? Kwa jinsi walivyo wadogo, ndivyo itakavyokuwa rahisi kwao kukabiliana na mazingira. Kwa vijana, mabadiliko yanaweza kuwa magumu sana. Zungumza nao na kupitia uongozi wako ili kuwaandaa.
- Shule: Kabla ya kwenda, ni vizuri kujua fursa za elimu zilizopo kwa ajiri ya watoto wako. Unaweza kuhitajika kuleta vitabu vya shule. Gharama lazima zizingatiwe. Uwe na hakika kwamba watoto wako wanaweza kupata elimu wanayohitaji kwa wakati ujao.
- Lugha: Je, watalazimika kujifunza lugha mpya katika eneo jipya? Je ni lugha gani mtaizungumza nyumbani kwako? Je, unataka wawe na ufasaha wa lugha mama? utahitaji kuwa na juhudi na kujitolea kwa upande wako ukiwa mzazi.
- Marafiki: Je, utaungana na timu ya wamishenari? Kama ndivyo je wana watoto? Je, kuna watoto wazawa wa mahali hapo ambao wanaweza kujenga urafiki nao?
- Nyumbani: Ni eneo gani utaenda kuishi? Je, utaishi katika eneo la vijijini, ilihali awali uliishi mjini? Je itakuwaje kwa watoto wako tokana na tofauti hiyo?
- Huduma za matibabu: Je, unajua namna utakavyopata huduma za afya kwa watoto wako ndani ya makazi mapya? Je, watoto wako wana mahitaji yoyote maalum ya kiafya? Ni kwa namna gani utalipia gharama za afya?
- Dharula: Je, misheni yako au ubalozi wa nchi yako utakusaidia iwapo kutakuwa na mgogoro wa kisiasa au janga la asili katika eneo lako jipya la huduma?
- Kiwango cha maisha: Ni hali gani ungependa zaidi uweze kuwa nazo kwenye mazingira mpya, iwe juu au chini kuliko vile ambavyo watoto wako wamezoea? Utawaandaaje watoto wako kwa viwango tofauti ya maisha?
- Familia: Je, watoto wako wana uhusiano gani wa karibu na binamu, shangazi na wajomba au babu na bibi? Je una mpango gani wa kudumisha uhusiano huu kutokea mbali? Je unaweza kupiga simu za intaneti mara kwa mara.
- Vitu vyenye thamani: Je! mtoto wako ana vitu vya thamani kama vile wanasesere, michezo, au nguo ambazo wanataka kwenda nazo? Ni vizuri kuzungumza nao kuhusu mapungufu na kuwapa uhuru wa kuchagua, ili waweze kuona kuwa nao ni wahusika katika maamuzi ya wa jambo hili jipya kwa ajili ya familia.
Kulikuwa na mafunzo kwa wamishenari wapya waliofika kutumika nchini Burkina Faso. Watoto katika familia moja walikuwa wameambiwa na wazazi wao kwamba wanaweza kuchagua kitu kimoja au viwili maalumu kutoka nchini kwao ili kuvileta nchi mpya waliyohamia. Wazazi waliwaahidi kufungasha vitu hivi na kwenda navyo Burkina Faso. Je unajua mtoto mmoja alichagua nini? Aliokota mawe madogo madogo kutoka nchini kwake! Kwa hiyo kokoto hizi muhimu zilifungwa na kufika na mizigo huko Ouagadougou, kama ilivyoahidiwa.